30 January, 2016

Stephane Mbia amejiunga na klabu ya Hebei China Fortune nchini Uchina

Stephane Mbia
Nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Stephane Mbia amejiunga na klabu ya Hebei China Fortune nchini Uchina.
Mbia amekuwa akichezea Trabzonspor ya Uturuki.
Mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 29 sasa atajiunga na nyota wa Ivory Coast Gervinho katika klabu hiyo ya Uchina.Gervinho alijiunga na Hebei China Fortune akitokea AS Roma Jumatano.Mbia
"Twamsubiri sana beki kamili Mbia afike hapa na kuonyesha ustadi wake,” klabu hiyo iliandika kwenye Twitter.Mbia aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Najivunia kujiunga na Hebei China Fortune, niko tayari. Twende kazi."

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...