06 September, 2016

Tecno kutoa Phantom 6 Septemba hii, itathibitisha ubora wake?


Tecno1.PNGSio suala jipya kwamba Bara la Afrika limegubikwa kwa kishindo na ulimwengu wa Smartphone (vijana wa mjini wanaziita simu janja). Ulimwengu huu umeshuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknojia kwenye simu za mkononi. Urahisi huu umeonekana kwenye manunuzi, mahusiano, ajira, kupata taarifa kwa haraka zaidi n.k. Kampuni kubwa ya kutengeneza simu, TECNO, imegusia mwendelezo wa simu zake kali za PHANTOM mwezi wa Septemba.

Nimefuatilia kwa makini matoleo ya PHANTOM na kugundua kwamba bidhaa zao zimekuwa zikiwalenga watumiaji wa maisha ya kati. Sasa wanagusia kwamba toleo lao jipya litawalenga watumiaji wa maisha ya juu.

Swali linakuja... Je! Wataweza kuliteka soko Septemba hii? Kwa jinsi mambo yanavyoonekana, lengo hili linaweza kufikiwa au kuvukwa.

TECNO PHANTOM 6 itakuwa nit oleo jipya la TECNO lenye vitu vingi vya kuangaliwa katika teknolojia nzima ya utengenezaji wa Samrtphone

Betri inayochaji kwa haraka
Huu umekuwa ni wimbo wa taifa kwa watumiaji wa Smartphone. Sawa, kuna vitu vingi vya kufurahia lakini tatizo linakuja kwamba simu haikai na chaji sana. Inapokuja kwenye PHANTOM 6, port yake ya Type-C 2.0 USB ina uwezo wa kuchaji simu yako kutoka 0% mpaka 35% ndani ya dakika 10 tu.

Kamera ya mbele (13MP) + Kamera ya nyuma (5MP) 
  Sasa hapo ni mwendo wa kutwanga selfies na picha kali ukiwa na kamera zenye uwezo wa hali ya juu mbele na nyuma. Picha hizi zenye ubora wa kipekee zinazoongeza rangi na uhai kwenye matukio yako ya kukumbukwa huku zikikutoa mwakemwake kama vile haujapatwa na jua.
Muundo wa chuma
Habari nilizozipata kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika ni kwamba, TECNO Phantom 6 itakuwa na ‘kava’ la chuma lilitengenezwa kwa umahiri wa hali ya juu na watu wanaoipenda kazi yao.

Umbo Jembamba


Inasemekana kuwa TECNO Phantom 6 itakuwa miongoni mwa simu nyembamba zaidi kutengenezwa duniani. Yaani utafikiri aliyekuwa anabuni muundo alikuwa kwenye ‘diet’

Bei
Ingawa TECNO Phantom 6 inategemewa kuwa ni miongoni mwa Smartphone zenye ubora wa hali ya juu, wataalamu wa mambo wanasema kwamba bei yake haitapishana na mfuko wa mwananchi.

cc TECNO TZ

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...