30 September, 2016

Europa League: Manchester United waichapa Zorya Luhansk

Zlatan Ibrahimovic
Manchester United wameondoka kwenye mkia kundi lao la ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, baada ya kupata ushindi dhidi ya Zorya Luhansk.

Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la pekee dakika ya 69, baada ya kombora la nguvu mpya Wayne Rooney kugonga mlingoti wa goli.

Hilo ndilo bao la kwanza la Ibra katika mechi tano, na lilitokana na kombora la kwanza la United lililolenga goli kwenye mechi hiyo.

United walitawala pakubwa mchezo huo uliochezewa Old Trafford, ingawa Sergio Romero alihitajika kufanya kazi ya ziada kuzima kombora la Paulinho muda mfupi kabla ya Ibrahimovic kufunga.

Mashetani hao Wekundu walitarajiwa kufanya vyema Europa League lakini walianza kampeni yao kwa kulazwa 1-0 na klabu ya Feyenoord ya Uholanzi mechi yao ya kwanza.

United sasa wamo nambari tatu kundini, wakiwa na alama sawa na Feyenoord na moja nyuma ya viongozi Fenerbahce wa uturuki ambao watazuru Old Trafford 20 Oktoba.Wayne RooneyUnited watarejea uwanjani Jumapili Ligi ya Premia ambapo watacheza dhidi ya Stoke City dimba la Old Trafford.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...