30 September, 2016

All the way Up Rmx- Diamond Plutnum Part 2


Diamond ameachia verse nyingine ya Remix yake ya ‘All the way Up’ , amejibu tetesi za kuchepuka, jina la Simba na mpinzani wake, Alikiba.
Kulikuwa na tetesi kuwa muimbaji huyo wa ‘Salome’ amerudiana na Wema sepetu kimyakimya, pia kuna tetesi kuwa amechepuka na Hamisa mobetto ambaye pia ametokea kwenye video yake mpya, Jibu ndio hili


“Mara nakula hamisa mobetto, ati Sepenga kaja magetho, ilimradi Zari apate mchecheto, Tale waambie waache unambinambi hata nikila wote dini yangu sio dhambi” 
Diamond na Alikiba ni washindani wakubwa kimuziki na maneno ya hapa na pale hayakosekani, Huku Diamond akiwa amesaini dili kubwa zaidi la kuwa balozi wa Vodacom, Alikiba na yeye alipata dili la kuwa Balozi wa Wild Aid, inayopinga mauaji ya tembo. Diamond nalo kaliongelea


“Siachi pengo hadi waombe poo, wao wakipost tembo si tunapost show”
Kama unajiuliza Tilalila ni nani, basi jua kuwa ni Mr.Blu jina limetokana na wimbo wake wa ‘Tilalila’ wa muda kidogo, Mr. Blu na Diamond waliwahi kuingia kwenye mgogoro wa jina la ‘Simba’, Chibude nalo hajaliacha lipite,
Mwambie na tilalila, kamwe kanzu haifanani na dera”
Enjo All the Way Up rmx

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...