23 May, 2016

Timu za mitandaoni zisiwe chanzo cha kuiangusha Bongo Flava.


 


Leo nimepanda hapa MTOKAMBALI nikiwa na jambo moja tuu lakuzungumzia. Kwa muda mrefu sasa tangu muziki wa Bongo flava kuanza kujulikana kimataifa, kumekuwako na timu tofauti tofauti katika mitandao ya kijamii na hata huku mitaani ambazo zimekuwa ziki support baadhi ya wasanii na kuponda wasanii wengine ambao ni wapinzani. 

Jambo hili linaonekana kuvuka mipaka kwa sasa maana chuki imekuwa ikionekana kati ya makundi hayo kana kwamba ni majeshi ya nchi fulani yakipigana na majeshi ya nchi nyingine.

Ifahamike kwamba, Muziki huu wa Bongo Flava bado ni mchanga(Mdogo) na zaidi ya yote ni yatima. Nasema hivyo kwa maana ya kwamba bado hatuja fikia pale tunapo takiwa kufika kama vile pale walipo fika wenzetu Nigeria, Uganda, Africa kusini na mataifa mengine ya Africa yenye Muziki unao watambulisha, licha ya Baadhi ya Wasanii wa hapa nyumbani kuonyesha kufanya vizuri kimataifa na kitaifa.

 Wasanii wa hapa nyumbani wamekuwa wakipambana vilivyo kila kukicha ili kuufanya muziki huu kufika pahala stahiki ila kuna baadhi ya watu hawapendi kuziona jitihada hizo na badala yake wamekuwa wakiwarushia vijembe wasanii hao na kutowapa support.

By the way simaanishi kwamba hawapewi support, ila suport inayo tolewa ni ile inayotoka upande wa team yake na ile kidogo inayo toka kwa wale wasio na team. Unaweza ukanipinga katika hili ila huu ni ukweli, na Ukiona hali hii haipo kwako, basi tambua kwamba huna team( ha ha haa).

 Lengo langu mimi ni kwamba, hizi team zilizoko kwa sasa zitambue ya kwamba muziki huu wa Bongo Flava ni wetu sote, hajalishi ni msanii wa team ipi ama ipi anaye imba, wote wanaimba Bongo flava. Na sioni haja ya kuwa na chuki katika hili maana Muziki sio vita wala ugomvi. Muziki ni dawa, muziki ni Faraja na Muziki ni Burudani tosha na zaidi ya yote muziki ni darasa huru katika jamii.

Nashangaa eti leo hii mtu ana dhiriki kumtukana msanii wa team ya pili pasipo kutambua ya kwamba hata huyo msanii wa team yake asinge hit kama huyo wa team pinzani asinge kuwako. Huu ni ulimbukeni usio kuwa na sababu na kama ni hivyo basi hakuna haja ya Wasanii hao kuimba bongo flava na badala yake kila team iunde style yake ambayo itatumika kama identity ya msanii huyo. mfano Team XXX watengeneze muziki wa aina yao na Team YYY wawe na yao na Tuiche bongo Flava yetu ikidunda kwa raha zake.

Ni hayo tuu kwa leo, ila tafadhali sana, heshima ya Bongo Flava iwepo. Bongo flava imeanzia mbali, tangu enzi za Kina marahem Complex, Mr two(sugu), sogy dogy, makundi kama vile East Coast team, watengwa, Dojo na Domo Kaya, Daz Nundaz na wakali wengine kibao walio isukuma bongo flava mpaka hapa ilipo. 

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...