Shirikisho la Mpira wa Kikapu ( NBA)
litazindua rasmi msimu wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana
kwenye kituo cha vijana cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dar
es Salaam mnamo tarehe 27 Februari mwaka huu.
Sherehe hii ya
ufunguzi wa mashindano hayo itahudhuriwa na Mchezaji Nyota wa mchezo huo
na Mwandamizi wa shirikisho la Mpira wa kikapu Ulimwenguni Allison
Feaster utakuwa ni uzinduzi rasmi wa ligi ya Mpira wa Kikapu kwa Vijana
wenye umri kati ya miaka 12 na 14.Ligi hii itajumuisha shule zipatazo thelathini (30) kutoka maeneo ya karibu na kila shule ikiwakilisha moja wapo ya timu 30 zinazoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani.
Ligi ya mpira wa kikapu ya vijana (Jr. NBA League) ni ligi ya NBA ya dunia inayoshirikisha mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana, wavulana kwa wasichana na inafundisha stadi za msingi za mchezo wa mpira wa kikapu pamoja na maadili muhimu ya mpira wa kikapu kwa wachezaji wanaoanza, Lengo likiwa ni kusaidia kukuza na kuboresha uzoefu wa Wachezaji, Makocha na Wazazi.
No comments:
Post a Comment