Klabu ya soka ya Barcelona imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 2-0
dhidi ya Arsenal katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Mtoano ya Timu 16
ya klabu bingwa barani ulaya (UEFA) mchezo uliopigwa uwanja wa Emirates.
Mabao ya Barcelona katika mchezo huo yamefungwa na mchezaji Lionel
Messi dakika ya 71 na Dakika ya 83 likiwa ni bao la pili lililofungwa
kwa njia ya penati .
Katika mchezo mwingine Juventus wakiwa nyumbani dhidi ya Buyern
Munich, mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kufuatia
sare ya kufungana mabao 2-2.
Bayern Munich ndio walioanza kuzigusa
nyavu za wapinzani kwa kuandika bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji
wao Thomas Muller dakika ya 43, muda mchache baadaye Arjen Robben
akaandika bao la pili kwa buyen Munich katika dakika ya 55 kipindi cha
pili.
Kwa upande wao Juventus walizinduka na kuandika bao la
kwanza kupitia kwa Paulo Dybala ikiwa ni dakika ya 63 kipindi cha pili,
huku Stefano Sturaro akiandika bao la pili la kusawazisha dakika ya 76
na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya kufungana bao 2-2.
Michuano
hiyo itaendelea tena Jumatano kwa Mechi 2 Dynamo Kiev ikiikaribisha Man
City huko Ukraine na PSV Eindhoven wao watakuwa Wenyeji huko Uholanzi
dhidi ya Atletico Madrid
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment