04 February, 2016

Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imefuzu kwa fainali ya mchuano wa CHAN


Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ilijikatia tikiti ya fainali baada ya kuilaza Guinea mabao 5-4 kwa mikwaju ya penalti.
Mechi hiyo ilikuwa imeishia sare ya moja kwa moja katika muda waziada baada ya Ibrahim Sankhon kuisawazishia Guinea kunako dakika ya mwisho ya kipindi cha pili cha muda wa ziada.
Lakini dalili za kufuzu zilionekana mapema,Ibrahim Bangoura alipokosa penalti ya kwanza ya Guinea.
Kimwaki,Mika,Jonathan Bolingi,Gikanji,Mechak Elia walifungia Leopards ya DRC huku
Ibrahim Sankhon,Leo Camara,Kile Bangoura,Daouda Camara wakiifungia Guinea.
Hata hivyo Kipa nambari moja wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Vumi Ley Matampi aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Youla na kuipa DRC ushindi wa mabao 5-4 Guinea
Timu hizo zilitoshana nguvu muda wa kawaida na mechi ikaingia muda wa ziada uwanjani Amahoro, Rwanda.
Ni katika muda wa ziada ambapo Jonathan Bolingi Mpangi kunako dakika ya 101 alifanikiwa kutikisa wavu wa Guinea.
Mapema kwenye mechi, mchezaji wa DR Congo Padou Bompunga alipewa kadi ya njano dakika ya 38. Hili lina maana kwamba hataweza kucheza fainali iwapo timu yake itafuzu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...