22 February, 2016

FA:Chelsea yaichapa Man City 5-1


Michuano ya kombe la FA iliendelea tena usiku wa jana kwa michezo mitatu, Chelsea wakicheza uwanja wao wa nyumbani Stamford Bridge walifanikiwa kuwachapa Manchester city mabao 5-1.
Magoli ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na wachezaji Diego Costa , Willian borges , Gary Cahill ,Eden Hazard , na bao la tano lilifungwa na mchezaji Bertrand Traore dakika ya 89 ya mchezo. Bao la Manchester city lilifungwa na mchezaji David Faupala .
Katika Michezo mingine Blackburn Rovers ilichapwa na West Ham bao 5-1 , huku Tottenham wakifungwa na Crystal Palace bao 1-0.
Kwa matokeo hayo sasa Chelsea itamenyana na Everton katika mchezo wa Robo Fainali baada ya kuiondoa Manchester City, Crystal Palace wakiongozwa na Emmanuel Adebayor wao watasafiri kuikabili Reading , Watford
watakuwa wageni kati ya Arsenal au Hull City na West Ham United itasafiri kuifuata Shrewsbury Town au Manchester United.
Arsenal watarudiana na Hull City kusaka hatua ya Robo Fainali, baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Emirates jana, wakati Shrewsbury Town wataikaribisha Manchester United kesho Uwanja wa New Meadow kuanzia Saa 4:45 usiku.
Mechi hizo za Robo Fainali zitachezwa wikiendi ya Machi 11 na 14 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...