Shungi la nywele ya msanii nguli wa
muziki chapa Rock na muanzilishi wa kundi la ''The Beatles'' John
Lennon aliyeaga dunia miaka 36 iliyopita imeuzwa kwa dola elfu
thelathini na tano ($ 35,000) katika mnada mmoja huko Marekani.
Kinyozi
wa Muimbaji huyo maarufu kote duniani alificha shungi la nywele baada
ya kumnyoa msanii huyo alipokuwa akijiandaa kuigiza katika filamu moja.Lennon aliuuawa mwaka wa 1980 mjini New York Marekani.
Mnunuzi mmoja shabiki sugu wa Lennon kutoka Uingereza ndiye aliyeandika hundi hiyo ya dola ($ 35,000).
Bidhaa zingine zilizotumika na kundi hilo la muziki la ''The Beatles''pia ziliuzwa katika mnada huo huko Texas.
Baadhi ya bidhaa hiyo ilikuwa nakala maalum ya albamu yao ya 'Yesterday and Today', iliyouzwa kwa dola laki moja u nusu ($150,000).
CHANZO; BBC
No comments:
Post a Comment