Mcheza Tenisi Rafael Nadal jana
alishindwa kutinga katika hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya Tenisi
ya ATP baada ya kupoteza mchezo kwa seti tatu kwa Mruguay Pablo Cuevas
katika mashindano ya wazi ya Rio .
Mshindi huyo wa mara 14 wa
Grand Slam alianza kwa kuongoza kwa pointi mbili kwa seti mbili lakini
baadaye alianza kupoteza mchezo kwa kufungwa jumla ya 6-7 (6) 7-6 (3)
6-4.Pamoja na kupoteza mchezo huo Nadal amesema amekubali kushindwa na atajaribu kulifanyia kazi na kubadili mwelekeo.
Cuevas ambaye anashikilia nafasi ya 45 ulimwenguni atakutana na Guido Pella katika hatua ya fainali.
No comments:
Post a Comment