Gazeti la kiswiss la Neue Zürcher Zeitung leo limeripoti kwamba Elneny ameshindwa kufanya mazoezi na Basel wiki hii. Hii ndio mara ya kwanza timu inakutana baada ya mapumziko ya kipindi cha sikukuu.
Neue Zürcher Zeitung linaripoti kwamba Elneny yupo njiani kwenda kujiunga na Arsenal.
FC Basel pia nao wametoa ishara kwamba uhamisho huo upo karibuni.
Klabu hiyo ya Uswiss imeandika kwenye mtandao wake rasmi kwamba – ‘kunaweza kuwa na uhamisho wa mchezaji wao katika siku za hivi karibuni.’
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali ni kwamba Arsenal watalipa kiasi cha 5 million euros kwa mabingwa hao wa Uswis, ada ambayo inaweza kwenda kufikia kiasi cha 7 million euros.
Elneny tayari ameripotwa kufanyiwa vipimo vya afya na ARSENAL – na kocha Arsene Wenger alimzungumzia mchezaji huyo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle.
No comments:
Post a Comment