Hatimaye kocha Pep Guardiola leo amethibitisha rasmi kwamba ataenda
kufundisha soka katika ligi kuu ya Uingereza – Barclays Premier.

Boss
huyo wa Bayern Munich leo alikutana na waandishi wa habari katika
mkutano wake wa kwanza wa 2016, na hakuweza kulikwepa swali kuhusu hatma
yake baada ya kuondoka Bayern mwishoni mwa msimu.
Bila kukwepesha maneno kocha huyo mwenye umri wa miaka 44, alisema:
“Nataka kufundisha soka katika ligi kuu ya England – Premier League.”

Guardiola
anapewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini Man City
Ikiwa tetesi zilizopo kwenye vyombo vya habari vya Ujerumani ni za
kweli.
Lakini Guardiola amesisitiza kwamba mpaka hajafikia makubaliano na
timu yoyote ya Premier League – Ingawa kuna vilabu kadhaa vimeshaanza
kumtumia ofa za kujiunga navyo.
No comments:
Post a Comment