05 January, 2016

Video: Huyu ndio Fellipe Anderson – Mbrazil Ambaye Anatajwa Kuelekea Old Trafford

Hatimaye dirisha la usajili limefunguliwa rasmi barani ulaya na tetesi za usajili ndio habari kuu katika kurasa za michezo za magazeti mbali mbali barani humo. Leo hii siku 4 baada ya dirisha kufunguliwa, gazeti la kiitaliano la  Gazzetta dello Sport leo limeripoti kwamba klabu ya Lazio imepunguza rasmi bei ya kumuuza kiungo wao Felipe Anderson – mchezaji ambaye anatajwa kutakiwa na klabu ya MANCHESTER United. Kabla ya mashabiki wa United kuanza kuwa na matumaini ya kumsajili Anderson, swali la kujiuliza ni kwanini Lazio wamekubali kushusha bei ya mchezaji huyo? Je ni labda mwanasoka huyo sio mzuri kama watu wanavyomchukulia? 1676247-35523523-1600-900Mbrazil huyo alikuwa na msimu mzuri sana wa 2014-15, alifunga magoli 10 katika mechi 32 za Serie A, lakini msimu huu mambo hayamwendei vyema kabisa – hajafunga goli lolote tangu October 2015. Mchezaji huyo wengi wanamuelezea ameshuka kiwango msimu huu, na sasa Gazzetta, wanaripoti kwamba Lazio wapo tayari kupokea kiasi cha 50 million euros kutoka kwa Man United ili kumuuza Anderson. Gazzetta wanaamini ofa rasmi itatumwa hivi karibu kutoka Old Trafford. 

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...