08 January, 2016

SAMATTA NDIYE MWANASOKA BORA ANAYECHEZA AFRIKA, AUBAMEYANG AMBWAGA YAYA TOURE

ORODHA KAMILI YA WASHINDI
MCHEZAJI BORA WA AFRIKA - Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon)
MCHEZAJI BORA ANAYECHEZA AFRIKA – Mbwana Aly SAMATTA
MCHEZAJI BORA WA KIKE - Gaelle ENGANAMOUIT (Cameroon)
MCHEZAJI BORA KIJANA - Victor OSIMHEN (Nigeria)
MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA VIZURI - Etebo Peter OGHENEKARO (Nigeria)
KOCHA BORA WA MWAKA- Herve RENARD (Ufaransa) – Kocha wa zamani wa Ivory Coast
REFA BORA WA MWAKA - Bakary Papa GASSAMA (Gambia)
TIMU BORA YA TAIFA – Ivory Coast
TIMU BORA YA TAIFA YA WANAWAKE- Cameroon
KLABU BORA YA MWAKA - TP Mazembe (DRC)
GWIJI WA AFRIKA - Charles Kumi GYAMFI (Ghana)
Samuel MBAPPE LEPPE (Cameroon)

KIKOSI BORA AFRIKA
Kipa: Robert Muteba KIDIABA (DRC)
Mabeki: Serge AURIER (Ivory Coast), Aymen ABDENNOUR (Tunisia), Mohamed MEFTAH (Algeria)
Viungo: Andre AYEW (Ghana), Yaya TOURE (Ivory Coast), Sadio MANE (Senegal), Yacine BRAHIMI (Algeria),     
Washambuliaji: Mbwana Aly SAMATTA (Tanzania), Pierre-Emerrick AUBAMEYANG (Gabon), Baghdad BOUNEDJAH (Algeria) 

WACHEZAJI WA AKIBA;
Djigui DIARRA (Mali)
Azubuike OKECHUKWU (Nigeria)
Kelechi NWAKALI (Nigeria)
Zinedine FERHAT (Algeria)
Adama TRAORE (Mali)
Victor OSIMHEN (Nigeria)
Kermit ERASMUS (Afrika Kusini)
Mbwana Samatta akipokea tuzo yake ukumbi wa mikutano wa kimataifa mjini Abuja

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza Afrika katika sherehe zilizofanyika usiku huu ukumbi wa mikutano wa Kimataifa mjini Abuja.
Samatta amepata pointi 127, mbele ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, kipa Robert Muteba Kidiaba wa DRC, aliyepata pointi 88, wakati mshambuliaji wa Etoile du Sahel ya Tunisia na timu ya taifa ya Algeria, Baghdad Bounedjah amepata pointi 63.
Mafanikio ya Samatta anayeweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo kubwa ya Afrika, yanakuja baada ya kuiwezesha Mazembe kutwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake nane. 
Mshambuliaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mara ya kwanza. 
Mchezaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani mwenye umri wa miaka 26, amewaangusha Yaya Toure wa Ivory Coast aliyekuwa anashikilia tuzo hiyo na Andre Ayew wa Ghana.
Amekusanya pointi 143, saba zaidi ya Toure wakati Ayew ameshika nafasi ya tatu kwa kupata pointi 112 na anakuwa mchezaji wa kwanza wa 
Gabon kushinda tuzo ya CAF
Kiungo wa Nigeria, Etebo Peter Oghenekaro ameshinda tuzo ya Mchezaji Anayechipukia Vizuri dhidi ya Mnigeria mwenzake, Azubuike Okechukwu, kipa wa Mali, Djigui Diarra, Mahmoud Abdelmonem Abdelhamid ‘Kahraba’ wa Misri na Mualgeria, Zinedine Ferhat.
Etebo, anayechezea timu ya Ligi Kuu ya Nigeria, Warri Wolves, aling’ara katika michuano ya U-23 ya Afrika Desemba nchini Senegal, akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake matano, yakiwemo mawili aliyofunga katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Algeria katika fainali.
Mshambuliaji kinda wa Nigeria, Victor Osimhen ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora Chipukizi akimshinda ndugu yake, Kelechi Nwakali, wachezaji wawili wa Mali, Adama Traore na Samuel Diarra na Yaw Yeboah wa Ghana.
Osimhen anayeshinda tuzo hiyo siku tisa tangu asherehekee kufikisha miaka 17 ya kuzaliwa, mafanikio hayo yanafuatia kufanya kwake vizuri katika Kombe la Dunia la U-17 Oktoba mwaka jana nchini Chile, akifunga mabao 10 na kuibuka mfungaji bora sambamba na kushinda Mpira wa Fedha baada ya Mchezaji Bora wa pili wa michuano hiyo, huku Nigeria ikitwaa Kombe.
Anakuwa mchezaji wa pili wa Nigeria kushinda tuzo hiyo baada ya Kelechi Iheanacho mwaka jana.
Mfaransa, Herve Renard ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa mara ya pili, baada ya kuipa Ivory Coast ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Equatorial Guinea.
Mfaransa huyo amewashinda Baye Ba wa Mali U-17, Patrice Carteron wa TP Mazembe, Faouzi Benzarti wa Etoile du Sahel na Emmanuel Amunike wa Nigeria U-17.


Renard, ambaye alishinda tuzo ya kwanza baada ya kuipa Zambia ubingwa wa Afrika mwaka 2012, alikabidhiwa tuzo yake na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Adoum Djibrine.
Cameroon imezishinda Ghana, Afrika Kusini na Zimbabwe katika kipengele cha timu bora ya taifa ya wanawake, wakati Ivory Coast imeziangusha 
Ghana, Mali U-17, Nigeria U-17 na Nigeria U-23 katika timu bora ya taifa ya wanaume.
Refa wa Gambia, Papa Bakary Gassama ameshinda tuzo ya refa bora kwa mara ya pili mfululizo akiwaangusha Ghead Zaglol Grisha wa Misri, Janny Sikazwe wa Zambia na Eric Arnaud Otogo Castane wa Gabon. 
Mualgeria, Haimoudi Djamel pia alishinda tuzo hiyo mara mbili mfululizo mwaka 2012 na 2013.
Kocha wa United Louis van Gaal anataka kusajili mshambul

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/01/manchester-united-yaambiwa-isahau.html
Copyright © saluti5

Latest 10:49 PM YANGA YAISHIKISHA ADABU MTIBWA MAPINDUZI CUP NA KUTINGA NUSU FAINALI KWA KISHINDO ...Azam yapewa mkono wa kwaheri Home » SOKA » MANCHESTER UNITED YAAMBIWA ISAHAU KUMPATA SADIO MANE WA SOUTHAMPTON MWEZI HUU MANCHESTER UNITED YAAMBIWA ISAHAU KUMPATA SADIO MANE WA SOUTHAMPTON MWEZI HUU A+ A- Print Email Mane knows he will have numerous options at top clubs in the summer, when Southampton will listen to offers Manchester United imeshindwa kumsajili mshambuliaji wa Southampton Sadio Mane mwezi huu. Louis van Gaal anataka kumsajili nyota huyo wa Senegal katika dirisha la Januari ili kuboresha safu yake ya ushambuliaji ambayo imepwaya kupita maelezo. Inasemekana maofisa wa United walibisha hodi Southampton wiki hii kujaribu kuwasilisha ombi lao la kumyakua Southampton. Lakini Manchester United wameambiwa hakuna biashara inayoweza kufanyika dirisha hili juu ya Sadio Mane labda kwa dirisha la kiangazi. Manchester United have failed in their bid to bring in forward Sadio Mane during the January transfer window Manchester United imenyimwa kumsajili Sadio Mane Southampton have rejected United's advances for the 23-year-old but will listen to offers in the summer Southampton imeigomea United kumyakua Sadio Mane United manager Louis van Gaal wants to add to his forward line with Mane seen as an ideal addition Kocha wa United Louis van Gaal anataka kusajili mshambuliaji mpya

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/01/manchester-united-yaambiwa-isahau.html
Copyright © saluti5

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...