19 January, 2016
Polisi nchini Kenya wamenasa noti bandia za jumla ya $693m (£485m) baada ya kufanya msako katika nyumba moja jijini Nairobi.
Watu wawili, mmoja kutoka Cameroon na mwingine kutoka Niger, wamekamatwa kuhusiana na pesa hizo.
Mkuu wa polisi Joseph Boinett akitangaza kupatikana kwa pesa hizo, amewaambia wanahabri kwamba hicho ni “kiasi kikubwa sana” cha pesa.
Amesema noti bandia za euro 369 milioni pia zimepatikana, pamoja na mitambo ya kutengeneza noti bandia.
Polisi walifanya msako baada ya kupokea habari za mfanyabiashara aliyetapeliwa Sh40 milioni za Kenya baada ya kuhadaiwa kwamba zingeongezwa mara tatu na kuwa Sh120 milioni.
Kwa jumla, pesa hizo zilizopatikana katika mtaa wa South C, zikibadilishwa na kuwa shilingi za Kenya zinafikia Sh110 bilioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni 2.3 za Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment