Akichapisha ripoti yake katika jarida la The Lancet, jopo la
wataalamu kutoka chuo cha afya mjini London limesema kumekuwa na
maendeleo finyu katika kupunguza idadi ya vifo vya watoto kabla ya
kuzaliwa licha ya kuwa vinaweza kuepukika.
Miongoni mwa taarifa za
kushangaza katika ripoti hiyo, ni kwamba itachukua zaidi ya miaka mia
moja na sitini kwa mwanamke wa kawaida anaetoka katika nchi za kusini
mwa jangwa la sahara kuweza kujifungua mtoto aliyehai kama ilivyo kwa
mwanamke katika nchi zenye pato la juu.
Katika nchi za kusini mwa
jangwa la sahara, utafiti huo unasema, asilimia sitini ya vifo vya
watoto wanaozaliwa vinatokea katika maeneo ya vijijini.
Katika
bara la Afrika, nchi ya Nigeria ndio inaongoza kwa idadi kubwa ya vifo
hivyo, huku ikiwa na zaidi ya vifo mia tatu katika kipindi cha miezi
mitatu iliyopita ya ujauzito.
Miongoni mwa habari njema ni nchi ya Rwanda ambayo imeweza kubadilisha mwelekeo na kupunguza idadi ya vifo hivyo.
Waandishi
wa ripoti hiyo wanasema, uboreshaji umefanyika zaidi katika afya ya
kina mama na vifo vya watoto, lakini sio katika kupunguza vifo vya
watoto ambao hawajazaliwa.
Wamesema, watoto hawapaswi kuzaliwa katika ukimya na wazazi wao hawapaswi kuomboleza kimya kimya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment