08 January, 2016

BAADA YA AZAM KUKWAMA MAPINDUZI CUP UVUMILIVU UMEMSHINDA HIMID MAO, AFICHUA MADUDU YALIYOIPONZA TIMU YAKE

Himid Mao
Kiungo wa kutumainiwa wa kikosi cha Azam FC Himid Mao amewapigia magoti mashabiki wa timu hiyo kutokana na timu yao kutupwa nje kwenye michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar baada ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu ya Mafunzo ya visiwani Zanzibar.
Himid ame-post ujumbe wa kuomba radhi kwenye account yake ya instagram na kukiri Azam imecheza kwa kiwango kibaya kupitiliza. Himid amekwenda mbali zaidi kwani amediriki kusema tangu amejiunga na timu hiyo hajawahi kuishuhudia Azam ikicheza kwenye kiwango duni kama ilivyokuwa kwenye mashindano ya Kagame na mechi mbili zilizopita za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Azam walijikuta wakiduwazwa na Mafunzo kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi B mchezo ambao Azam FC walihitaji ushindi ili kujiwekea matumaini ya kusonga mbele.
Huu hapa ujumbe wa Himid kwenda kwa mashabiki akiwataka radhi kwa kile alichokiita ni kiwango kibovu kuwahi kuoneshwa na timu hiyo.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki wote wa Azam FC kwa performance mbaya tuliyoionesha kwenye mashindano ya Mapinduzi na mechi mbili za ligi kabla ya kuja huku, matokeo ni sehemu ya mchezo inakubalika, lakini kitu kinachoangaliwa ni unapataje matokeo yawe mazuri au mabaya”.
“Tumepata matokeo mabaya kutoka kwenye performance mbaya zaidi kuwahi kuiona katika timu yetu tangu nilipoanza kucheza hadi sasahivi, nasikia aibu sana tena zaidi ya sana sina njia ya kuelezea ni kiasi gani najisikia vibaya na aibu naamini na wachezaji wenzangu wanajisikia vibaya kama ninavyojisikia mimi ….I will work as harder as I can to make things better for me and my team”.
Himid Mao 1
Azam imeondolewa kwenye mashindindano ya Mapinduzi Cup hatua ya makundi kwa mara ya kwanza tangu timu hiyo ilipoanza kushiriki michiuano hiyo.
Mafunzo imeivurumisha nje timu ya Azam ambayo imemaliza michezo yake ya makundi ikiwa  na popinti mbili huku ikiwa haijashinda mchezo hata mmoja zaidi ya kuambulia sare kwenye mechi mbili mechi ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar na mechi ya pili dhidi ya Yanga huku wakinyolewa na Mafunzo kwenye mchezo wao wa mwisho.
  
Source:Shafih Dauda


No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...