WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametoa siku saba kwa
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limpe sababu za kubadili mfumo wa
utunuku viwango vya ufaulu wa awali( Division) na kwenda wa wastani wa
pointi (GPA) unaotumika sasa Kidato cha Nne na Sita.
Aidha,
ametaka litoe maelezo ya kitaalamu juu ya sababu za kuanzisha mtihani wa
pili kwa watahiniwa wa kujitegemea na kwamba zisipomridhisha, mwaka huu
wasifanyishwe mtihani huo.
Mfumo
wa GPA ulianza kutumika kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa mwaka 2014
ambao matokeo yao yalitoka mwaka jana.Vile vile mitihani miwili kwa
watahiniwa wa kujitegemea, ilianza mwaka 2014 na 2015.
Ndalichako
ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa baraza hilo kwa miaka tisa,
alitoa maagizo hayo jana ambako pamoja na masuala mengine, alishuhudia
namna alivyojaribiwa na kuletewa vishawishi jambo ambalo alisema,
alilishinda kwa kusimamia taaluma.
Maagizo hayo aliyatoa
alipotembelea na kuzungumza na viongozi, wafanyakazi wa NECTA ambako
hakuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk
Charles Msonde.
Alisema tangu alipoteuliwa kuwa Waziri, amepokea
malalamiko mengi kutoka kwa wadau wa elimu na wananchi juu ya mfumo wa
sasa wa upangaji matokeo wa GPA ambao umekuwa haueleweki na kwamba
hawakushirikishwa katika mabadiliko hayo.
“ Nataka nijue
sababu za kitaalamu za kubadilisha mfumo wa upangaji wa matokeo kutoka
kwenye ule wa Division (madaraja) kwenda kwenye ule wa GPA na kama huo
mfumo una tija kwa elimu yetu,” alisema.
Awali , Dk Msonde
alisema mfumo huo ulipitishwa baada ya vikao kati yake, Tume ya Vyuo
Vikuu (TCU), Baraza la Vyuo vya Ufundi (Nacte) na Wizara.
Alisema
baraza lilitakiwa kuendesha mfumo huo ili kwenda na mifumo mingine ya
elimu ya juu katika kurahisisha udahili wa wanafunzi kwenda sanjari na
mfumo wa serikali mtandao na ajira.
Watahiniwa kujitegemea
Kuhusu uanzishwaji wa mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea, Ndalichako alisema, “Nataka
sababu za watahiniwa wa kujitegemea kupewa mtihani wa pili ambao
unachukuliwa kama alama upimaji endelevu kwa mwanafunzi.
“ Kama
baraza ambalo ndio wataalamu, mnasema mmeamua kutoa mtihani wa pili
kutokana na kupokea malalamiko ya kufeli na mtihani mgumu, basi hatuwezi
kuendelea nao, nataka nipate sababu za kitaalamu na kama sababu
haziridhisha basi mwaka huu wasifanyishwe mtihani wa pili,” alisema.
Alisema
kwa kawaida, mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea hauwezi kuwa
mbadala wa alama endelevu kwa wanafunzi. Alisema unaongeza mzigo kwa
watahiniwa na gharama za kulipa wasimamizi na wasahihishaji wa mitihani
hiyo.
Ashuhudia alivyojaribiwa
Ndalichako
aliwataka viongozi wa baraza hilo kutokukurupuka katika kutoa uamuzi na
kufanya mabadiliko yasiyo na tija kwa taifa. Badala yake, alisisitiza
watumie utaalamu wao kushauri na kukataa maagizo yasiyo na tija kusaidia
katika kuboresha elimu.
Katika hatua nyingine, Ndalichako
aliwataka watendaji wa Baraza hilo kufanya kazi yao kwa umakini na
uadilifu na kuepuka vishawishi. “ Baraza la Mitihani ni sehemu ngumu sana, hasa kutokana na kuhudumia watu na hasa katika suala zima la mitihani.
"Na ni eneo ambalo lina vishwishi vingi, hata mimi nilijaribiwa kuletewa vishawishi lakini nilisimama misimamo ya taaluma,” alisema.
Ndalichako pamoja na kuwapongeza Baraza kwa kutoa vyeti mbadala, ametaka kuwa makini katika suala hilo kuzuia udanganyifu.
Alisisitiza watoe tathmini ya kina katika matokeo ya wanafunzi ambayo yatasaidia wizara kufanya uboreshaji.
“Nilipokuwa hapa, kuna wakati nilikuwa nakosa usingizi linapokuja suala
la kutangaza matokeo, unakuta matokeo ya wanafunzi 30 yote ni mbaya,
sasa hapa si kuwa wanafunzi wote walikuwa hawafundishiki ila kuna tatizo
la ziada, na hilo ndio tunatakiwa kushughulikia,” alisema.
Alisema, “
Nilikuwa naumia sana na ubora wa elimu iliyokuwa ikitolewa kwa baadhi
ya shule, sasa nimepewa kazi ya kuhakikisha elimu inakuwa bora,
tunaondoa watu wa kuchora mazombi na ule wakati wa shule kugeuka vituo
vya kulelea watoto badala ya kutoa elimu umefika mwisho.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment