12 December, 2015

Victoria: Sina mpango na wanaume wa Kenya

post-feature-imageMSANII wa muziki nchini Kenya, Victoria Kimani, amesema hana mpango wa kuolewa na wanaume wa nchini Kenya kwa kuwa hawajui kukaa na wapenzi wao.

Mrembo huyo amesema wanaume wengi wa nchini humo wamekuwa tofauti na wale wa nchini Nigeria, hivyo ni bora aelekee huko kwa ajili ya kupata mwanaume bora ambaye atadumu naye.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika muziki mara baada ya kusaini mkataba mpya katika kampuni ya kusimamia kazi zake ijulikanayo kwa jina la Chocolate City Music Label, amesisitiza kwamba lengo lake kubwa ni kuolewa na mtu kutoka Nigeria.

“Wanaume wa Nigeria wanajua jinsi ya kuishi na mwanamke, wanaonyesha heshima ya hali ya juu na hivyo ndivyo ninavyotaka katika maisha yangu,” alisema Victoria.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...