Rais wa Argentina aliyemaliza muda
wake , Cristina Fernandez de Kirchner, amewaaga maelfu ya wafuasi wake
ambao walikusanyika katikati mwa mji wa Buenos Aires.
Katika
hotuba yake ambayo ilijaa hisia nje ya ikulu, Fernandez alivishutumu
vyombo vya habari vya nchi hiyo kwa kuipiga vita serikali yake ya mrengo
wa kushoto.Fernandez na mume wake ambae tayari ameaga dunia, Nestor Kirchner, wamekuwa madarakani kwa muda wa miaka kumi na mbili.
Ametetea hali ya uchumi, na kusema hakuna katika utawala uliopita ambao uliiacha Argentina bila madeni.
Na kuwataka raia wa Argentia kutetea haki zao na maslahi yao ambayo wameyapata.
Makundi yaliyokusanyika katika eneo hilo yalikuwa yakiimba wakati Fernandezi akipanda katika jukwaa.
No comments:
Post a Comment