Nyota wa Hollywood Samuel L Jackson
atahamia Afrika Kusini iwapo Donald Trump atashinda uchaguzi wa urais
Marekani, tovuti ya News 24 imeripoti.
Trump, mmoja wa wanaowania
tiketi ya kugombea urais Marekani kupitia chama cha Republican,
ameshutumiwa vikali baada ya kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia
Marekani.Haijabainika iwapo matamshi ya mwigizaji huyo, yaliyopeperushwa kwenye sehemu ya kipindi cha Jimmy Kimmel Live iliyorekodiwa awali Jumatatu, yalitolewa kabla au baada ya matamshi hayo ya majuzi zaidi kutoka kwa Trump.
Bw Trump, wakati mmoja amewahi kunukuliwa akikosoa kundi linalotetea haki za watu weusi Marekani la Black Lives Matter.
No comments:
Post a Comment