10 December, 2015

Rais Magufuli kaandikwa tena na tovuti ya gazeti la Uingereza, ni kuhusu Dec 9.


Sasa hivi sio habari mpya tena kuona gazeti au mtandao wa nchi flani maarufu duniani limemuandika Rais Magufuli wa Tanzania, tayari mpaka sasa tumeshaona Magazeti ya Australia, South Africa, Zimbabwe, Kenya, China, Uganda na Uingereza yamemuandika Dr. Magufuli.
December 9 2015 baada ya Rais Magufuli kuchukua headlines za yeye kufanya usafi, The Telegraph (telegraph.co.uk) wameandika mistari ambayo inaonyesha kabisa kitendo cha Dr. Magufuli kuingia mtaani kufanya usafi kimewagusa na ni tofauti na Waziri mkuu wa Uingereza ambaye sio rahisi kumuona au kufanya alichofanya Dr. Magufuli.
Kwenye sehemu ya stori yenyewe wamenukuu mistari ya Rais Magufuli kusema ni aibu kusherehekea siku ya uhuru Tanzania wakati nchi ina Wagonjwa wa kipindupindu ambapo kwenye taarifa hiyo ziliambatanishwa picha zikimuonyesha Rais JPM akifanya usafi.
magu 3
magu 2
Magu 1

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...