10 December, 2015

MSIKIE JULIO ANAVYOSEMA KUHUSU SHINYANGA DERBY

IMG-20150825-WA0015
Wakati macho na masikio ya wengi yakiwa yameelekezwa kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Simba SC utakaochezwa December 12 kwenye uwanja wa taifa, kule mkoani Shinyanga kutakuwa na bonge la derby kati ya Stand Unted ‘chama la wana’ dhidi ya Mwadui FC chini ya Super Coach Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ katika mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo amesema timu yake ipo katika maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo huku akikiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu na lolote linaweza kutokea japo ametamba kikosi chake kimejipanga kwa ajili ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
“Sisi tutacheza mchezo wa Shinyanga derby dhidi ya Stand United timu ambayo ilianza kupanda daraja kabla yetu sisi na mwaka unaofuatia sisi tukapanda. Ni watu wa mkoa mmoja lakini watu wenye upinzni na ushindani wa kimchezo kiasi ambacho naweza kusema mechi itakuwa ngumu na lolote linaweza kuokea lakini timu yangu ipo katika maandalizi mazuri, tumejipanga vizuri kwa ajili ya ushindi wa mechi hiyo”, amesema Julio.
“Nimemsajili Gabriel Emanuel kutoka timu ya JKT Oljoro na mwingine ni Ismail Gabo mchezaji ambaye tumempata kwa mkopo kutoka Azam FC kwahiyo nafikiri kutokana na wachezaji nilionao nikiongeza na hawa wawili nitakuwa na idadi kamili ya wachezaji watakaomalizia msimu huu wa ligi ya Vodacom”.
Mchezo huo unazikutanisha timu hizo huku Stand United ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 wakati Mwadui FC yenyewe ipo nafasi ya saba kwa pointi zake 15.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...