10 December, 2015

TIMU YAKABIDHI WACHEZAJI WAKE BODABODA

URA
Taasisi ya mapato nchini Uganda (URA) kupitia timu yake ya URA FC imewapa wachezaji wake zawadi ya pikipiki maarufu kama ‘bodaboda’ kwa ajili ya kuongeza vipato vyao mbali na mshara wanaoupata kila mwezi kutoka kwenye klabu yao.
URA imewasaidi wachezaji wake kwa kuwapa pikipiki hizo za biashara ‘bodaboda’ ambazo zimesambaa nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla kwa ajili ya kusafirisha abiria pamoja na mizigo.
Kutokana na hali ya maisha kupanda kwenye mji kuu wa Uganda Kampala, mwenyekiti wa klabu hiyo Ali Ssekatawa amesema kwamba, hawataki wachezaji wao wategemee mishahara pekee hivyo wakaona ni vyema kuwatafutia vyanzo vingine vya kupata pesa vitakavyowasaidia kujipatia kipato mbali na kazi yao ya kucheza mpira.
“Tunaangalia mfumo wa kuwafanya waweze kujitegemea wenyewe na tukifanikiwa katika hilo basi wachezaji wetu watacheza vizuri”, amesema Ssekatawa.
URA ni moja kati ya vilabu maarufu kwenye ligi ya Uganda (Uganda Premier League) na wamekuwa wakiwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki kwenye michuano ya CAF Champions League pamoja na ile ya Confederation Cup ambayo kwa pamoja ni michuano mikuwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.
Mapema mwaka huu commissioner wa URA FC Doris Akol aliahidi watawasaidia wachezaji kujipatia kipato cha ziada na mwenyekiti wa klabu Ssekatawa amekabidhi bodaboda 17 kwa wachezaji kwenye uwanja wa mazoezi.
Mchezaji liyedumu kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu na kuwahi kuitumikia timu ya taifa ya Uganda Simeon Masaba amesema amefurahishwa na hatua hiyo na itawasaidia wachezaji kupata kipato cha ziada kwa ajili ya familia zao.
Beki huyo aliongeza kuwa, japo biashara ya bodaboda ni hatari pamoja na wezi pia kuwaandama waendesha bodaboda, anaamini kama zitatunzwa na kutumiwa vizuri zitawasaidia wachezaji wa URA kama sehemu ndogo ya bishara yao.
Kocha wa timu hiyo Kefa Kisaala pia amepokea moja ya bodaboda hizo na kusema amefurahishwa na zoezi hilo.
Kwa upande wake kiungo wa timu hiyo Saidi Kyeyune yeye amesema, hakubaliani na mpango huo kwasababu anafikiri itakuwa ni vigumu ku-manage.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...