09 December, 2015

Mawaziri waidhinisha kura ya muda wa rais Rwanda

Kagame
Baraza la mawaziri Rwanda limeidhinisha kufanyika kwa kura ya mamuzi kuhusu marekebisho ya katiba yatakayomruhusu Rais Paul Kagame kuendelea kukaa madarakani.
Kikao cha baraza la mawaziri kimetangaza kuwa kura ya maamuzi kuhusu katiba hiyo mpya itafanyika tarehe 18 Desemba, ambayo ni Ijumaa wiki ijayo, kwa wananchi wa Rwanda na tarehe 17 kwa raia wa Rwanda wanaoishi ng’ambo.
Tangazo hilo la baraza la mawaziri limethibitisha pendekezo lililotolewa na wa mkutano mkuu wa chama tawala RFP mwishoni mwa wiki iliyopita wa kufanyika kwa kura hiyo haraka iwezekanavyo.
Marekebisho ya katiba tayari yamekwisha idhinishwa na bunge la Rwanda.
Kulingana na katiba mpya, Rais Paul Kagame baada ya kumaliza muhula wake mwaka 2017, atakuwa huru kugombea muhula wa tatu ambao utakuwa wa miaka 7 na baadaye kuruhusiwa tena kugombea mihula mingine miwili, kila mmoja ukiwa wa miaka 5.
Katiba iliyokuwepo ilikuwa inaweka ukomo wa mihula miwili pekee madarakanRFPMarekebisho ya katiba nchini Rwanda yamekwisha pingwa na baadhi ya nchi wafadhili wa taifa hilo kama vile Marekani, Uingereza na umoja wa nchi za ulaya kwa madai kuwa marekebisho hayo yanakandamiza demokrasia.
Hata hivyo, akijibu shutuma hizo, Rais Paul Kagame alisema kuwa kilichotokea nchini humo ni matakwa ya wananchi ambao bila shaka watapewa haki ya kudhihirisha hivyo kupitia kura ya maamuzi.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...