Vipi kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wasingekuwepo kwenye
soka?Umeshawahi kufikiria hilo, nini kingetokea na kipi kisingetokea?
Nimejaribu kukaa na kupata vitu saba ambavyo vingetokea kwenye ulimwengu
wa soka kama wafalme hawa wa soka la kizazi hiki wasingekuwepo kwenye
soka.
- Rekodi ya Gerd Muller Ingekuwa Hai

Gwiji
wa soka wa Gerd Muller alivunja rekodi ya Forenc Deak mwaka 1972 kwa
kufunga magoli 85 katika mwaka 1. Ni vigumu sana kuvunja rekodi ya namna
hii. Mpaka 2011, Ronaldo alikarbia kuivunja kwa kufunga magoli 60,
2012, Lionel Messi akaivunja rekodi hii kwa kufunga magoli 91. Hii ni
rekodi iliyoingia kwenye kitabu cha Guinness – rekodi ya Muller ingeweza
kuwa hai kama Messi asingekuwepo.
- Makombe matano ya Champions League kwa Manchester United

Manchester
United tayari wameshashinda makombe matatu ya Champions League. Moja ya
vikwazo vyao vikubwa katika kutwaa ubingwa huu zaidi imekuwa klabu ya
FC Barcelona. Katika fainali ya msimu wa 2008/09 na 2010/11 United
walikutana na barcelona na mara zote mbili wakapoteza. Mmoja wa mwiba wa
United katika fainali hizo alikuwa Lionel Messi na kama isingekuwa
Messi, labda United wangekuwa wameshinda Champions League mara 5 mpaka
sasa.
- Upinzani wa Gareth Bale vs Neymar Ungekuwa Mkubwa

Rekodi ya Real Madrid kushinda ubingwa wa wa 10 wa Ulaya – La Decima
ulifuatiwa na ujio wa Neymar katika klabu ya Neymar ndani ya Barcelona.
Kufikia hapo ukaanza ulinganishwaji kati ya Neymar na Gareth Bale na
ikahisiwa ungekuwa ushindani ambao ungeurithi au kuuondoa ushindani
Ronaldo versus Messi. Haikuweza kutokea hivyo, Ronaldo na Messi
wakakuza viwango vyao kwenda level nyingine na taratibu ushindani wa
kuwafananisha Bale na Neymar umepungua kabisa. Kama usingekuwepo wa
Messi na Ronaldo, battle ya Neymar na Bale ingekuwa kubwa sana kama
ilivyo sasa kati ya Ronaldo na Messi.
- Umuhimu zaidi wa Wayne Rooney

Kilikuwa
kipindi kigumu kwa Manchester United wakati Ronaldo alipoondoka
kwenda Real Madrid. Baada ya kuondoka CR7, alikuwa ni Wayne Rooney
aliyebeba majukumu na kujaribu kuziba pengo la Ronaldo. Rooneyamefanya
mengi tangu wakati huo na inasikitisha baadhi ya Man United bado hawampi
heshima anayostahili kwa makubwa aliyofanya tangu alipoondoka Ronaldo.
Bila uwepo wa Rooney katika miaka 6 iliyopita labda United isingepata
mafanikio waliyopata tangu kuondoka kwa Rooney. Mashabiki wa United
wamekuwa wakimhusudu Ronaldo kuliko wanavyompa heshima Rooney, mtu
unaweza kufikiria kama Ronaldo asingekuwepo labda Rooney angepata
umuhimu na heshima anayostahili.
2. Ushindani Zaidi Katika Ballon d’Or

Kuna
yoyote ambaye anakumbuka mara ya mwisho Tuzo Ya Ballon D’or imekuwa sio
baina ya wawili hawa? Kumbukumbu zinaonyesha ni mbrazil Ricardo Kaka
ndio mshindi wa wa tuzo miaka takribani sita iliyopita kabla Messi na
Ronaldo hawajaiteka tuzo hiyo na kuifanya yao.
Messi na Ronaldo wameifanya tuzo hiyo mashindano yao, hakuna mchezaji
mwingine aliyeonekana tishio kwao kwenye tuzo hiyo. Kama wachezaji hawa
wawili wasingekuwepo labda Fernando Torres, Sergio Aguero, Luis Suarez
au wachezaji wengine wangekuwa na nafasi ya kushinda Ballon d’Or.
1. Mchezo wa wa Football Usingekuwa Sawa. 
Kwa
namna tulivyoona matukio yote ya kisoka ambayo yangetokea kama Ronaldo
na Messi wasingekuwepo. Wawili hawa wamekuwa ni baraka kwenye soka –
wote wawili wameupa ulimwengu wa soka kumbukumbu tamu ambazo
tumezishuhudia. Wametupa ladha ya ushindani wa Pele na Maradona. Kwa
hakika kama wasingekuwepo soka lingekosa ladha nzuri waliyotupatia,
mabeki labda wangekuwa na urahisi wa kuzuia zaidi. Naamini wengi
miongoni mwetu tunajivunia kuwashuhufia viumbe hawa wawili katika
kipindi muongo mmoja uliopita.
No comments:
Post a Comment