Wakati klabu ya Simba ikiwa imefanya usajili katika kipindi cha dirisha dogo kuhakikisha inakiongezea nguvu kikosi chake, taarifa zinadai kwamba, wachezaji hao waliosajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo hawataruhusiwa kucheza kwenye mchezo dhidi ya Azam FC unaosukumwa jioni ya leo kwenye uwanja wa taifa .
Wachezaji hao hawatacheza kwasababu bado hawajathibitishwa na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya TFF ili waanze kuitumikia klabu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa inamatarajio ya kuwatumia wakali hao kutaka kuangamiza Azam.
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amesema kamati ya sheria na hadhi za wachezaji hukutana mara baada ya dirisha la usajili kufungwa kwa ajili ya kuidhinisha usajili wa wachezaji wa vilabu ikiwa ni pamoja na kupitia pingamizi zilizowekwa kwa wachezaji mbalimbali.
“Kanuni za usajili au kanuni za ligi zinasema klabu au timu inamuombea usajili mchezaji kwa TFF kwahiyo TFF ndiyo inaidhinisha usajili kwahiyo baada ya TFF kuidhinisha ndipo mchezaji anapata license au mchezaji anaweza akawa ameidhinishwa lakini hata hati ya uhamisho wa kimataifa lakini itakapofika tu acheze”, amesema Wambura.
“Lakini mpaka sasahivi kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ambayo ndiyo inathibitisha usajili haijakutana kwahiyo ikikutana watu wakapata license wanaweza wakacheza lakini kama hawajapata license ni wazi hawawezi kucheza mpaka kamati itakapokuwa imekaa”.
Lakini kamati mpaka sasa bado haijakutana kwahiyo wachezaji wote wa vilabu vyote (vinavyoshiriki ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza) waliosajiliwa katika dirisha dogo hawatakuwa na uhalali wa kucheza katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara itakayopigwa leo na kesho.
Kwahiyo wachezaji kama Brian Majwega, Paul Kiongera na Dany Lyanga hawata nafasi ya kucheza kwani hadi sasa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji bado haijakutana kuidhinisha uhalali wa wachezaji wote waliosajiliwa kwenye dirisha dogo na mara nyingi kamati hukuta mara baada ya dirisha la usajili kufungwa.
No comments:
Post a Comment