12 December, 2015

VAN PLUIJM AWATOA HOFU YANGA

Hans van der Pluijm, kocha mkuu wa club ya Yanga SC
Kocha mkuu wa mabingwa wa kikosi cha Yanga mholanzi Hans van Pluijm amewatoa hofu mashabiki na wachama wa Yanga juu ya wachezaji ambao ni majeruhi na kuwaahidi ushindi kutoka kwa kikosi ambacho kitacheza mchezo dhidi ya Mgambo JKT  kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo jioni.
Yanga itawakosa wachezaji wake muhimu kama nahodha wake Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela na mshambuliaji Donald Ngoma ambao wote ni majeruhi huku Haruna Niyonzima akiwa bado hajajiunga na kikosi hicho tangu aende kwao kukitumia kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda kwenye michuano ya CECAFA Challenge Cup.
“Kila kocha kocha ukimuuliza kuhusu mchezo ulioko mbele yake atakwambia anahitaji pointi tatu, tutafanya kila tunachoweza ili kuzipata pointi hizo, kwa bahati mbaya kikosi chetu kina majeruhi lakini tunakikosi cha wachezaji 24 kwahiyo wapo wengine wataochukua nafasi za hao ambao ni majeruhi”, hayo ni maneno ya kocha wa Yanga ‘kibabu’ Hans van Pluijm.
Nimeshawahi kuwanona wapinzani wetu Mgambo wakicheza mara kadhaa na ninafahamu jinsi wanavyocheza, wanacheza kwa kutumia sana nguvu lakini sisi pia tuna aina yetu ya uchezaji na tuko tayari kuwakabili.
Mgambo JKT wanatambulika kuwa ni wagumu hasa wanapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani na wamekuwa wakifanya mazoezi magumu kwa takribani mwezi mzima chini ya kocha wao ‘Mchawi Mweusi’ Bakari Shime wataingia uwanjali wakiwa full hawana mchezaji majeruhi hata mmoja huku kiungo wao Ali Nassoro Fudu akirejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa majeruri ya muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...