Filamu ya ucheshi kuhusu mkutano wa
kwanza wa kuchumbiana kati ya Barack Obama na Michelle ni miongoni mwa
filamu ambazo zitaonyeshwa kwenye maonyesho ya filamu ya Sundance 2016.
Filamu
hiyo kwa jina Southside With You inaigiza yaliyojiri adhuhuri moja
majira ya joto 1989 pale Obama alipomchumbia mkewe wa baadaye Michelle
Robinson, mjini Chicago.Filamu nyingine zitakazoonyeshwa ni Swiss Army Man, ambapo mwigizaji mashuhuri Daniel Radcliffe anaigiza kama maiti.
Makala ya 2016 ya maonyesho ya Sundance yatafanyika 21 hadi 31 Januari katika Park City, Utah.
Maonyesho hayo yaliasisiwa na mwigizaji Robert Redford.
Tika Sumpter anaigiza Michelle naye Parker Sawyers Bw Obama.
No comments:
Post a Comment