31 December, 2015

CUF kususia sherehe za mapinduzi Zanzibar

CUF
Chama cha Wananchi kimesema hakitashiriki maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi visiwani Zanzibar kutokana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi.
Chama hicho kupitia taarifa kimesema maadhimisho hayo yatafanyika “Serikali ikiwa inaongozwa na viongozi ambao hawana uhalali na ridhaa ya wananchi”.
“CUF tumesisitiza mara zote kwamba hatukubaliani na uamuzi (wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar),” inasema taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Mshauri wa Katibu Mkuu wa CUF Mansoor Yussuf Himid.
“Tunapenda kutumia fursa hii kuwaeleza wananchi wa Zanzibar kwamba viongozi wetu hawatoshiriki katika shughuli walizopangiwa katika ratiba ya sherehe hizi.”
Siku ya Mapinduzi huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Januari kukumbuka tarehe 12 Januari, 1964, siku ambayo Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ilitangazwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Serikali ya visiwani ilikuwa imetangaza ratiba ya kufanyika kwa shughuli mbali mbali zenye lengo la kuadhimisha Mapinduzi hayo kuanzia tarehe 2 Januari hadi kilele tarehe 12 Januari katika sherehe kuu Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.
“Kiuataratibu, kilele cha sherehe huongozwa na Rais ambaye yupo kikatiba. Kushiriki katika sherehe hizo ni kuhalalisha kipindi cha uongozi ambacho hakipo tena kikatiba,” taarifa ya CUF imesema.Mzozo
“Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wenziwe ndani ya Chama waliokuweko Serikalini hadi tarehe 2 Novemba, 2015 hawako tayari kuhalalisha uvunjaji wa Katiba ya Zanzibar ambayo ndiyo sheria kuu ya nchi.”
Mapema wiki hii, Chama cha Mapinduzi (CCM) kiliwataka wanachama wake wajiandae kwa marudio ya uchaguzi Zanzibar, hatua hiliyoshutumiwa na CUF.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...