31 December, 2015

Shilole afuta tattoo ya Nuhu Mziwanda iliyokuwepo kifuani kwake!

post-feature-imageKuna taarifa mtaani kuwa penzi la mastaa wa muziki, Shilole na Nuh Mziwanda limevunjika. Japokuwa sio mara ya kwanza kwa tetesi kama hizo kuhusu couple hiyo, lakini safari hii kuna dalili kuwa inaweza kuwa ‘serious’.

Picha ikionyesha tattoo mpya kifuani
Moja ya vitu vinavyoongeza nguvu ya tetesi hizo, Shishi amefuta ile tattoo aliyochora kifuani kwake miezi kadhaa iliyopita, yenye jina la ‘Nuh’ na kuchora UA juu yake.

Kipindi cha karibuni wawili hao hawaonekani pamoja kama ilivyozoeleka, na kila mmoja amefuta picha zao za pamoja kwenye akaunti zao za Instagram. Pia weekend iliyopita Shishi alifanya sherehe nyumbani kwake ambayo hakusema sababu ya sherehe hiyo, lakini hakuwa na Nuh na wala hakupenda kumzungumzia pale alipoulizwa na marafiki aliowaalika.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...