Wakati kukiwa na presha ya kuhakikisha timu yake inapata matokeo
chanya, baada ya mfululizo wa matokeo mabaya katika La Liga, Hali
inazidi kuwa tete kwa kocha Rafael Benitez baada ya maamuzi yake katika
upangaji wa kikosi kuiponza Madrid kuondolewa katika michuano ya Copa
Del Rey.

Kwa
mujibu wa taarifa kutoka gazeti la AS, miamba hiyo ya La Liga,
imeondolewa kwenye Copa Del Rey baada ya kumchezesha mchezaji
aliyefungiwa Dennis Cheryshev katika mechi ya michuano hiyo dhidi ya
timu ya daraja la pili Cadiz, jumatano iliyopita.

Cheryshev
alifunga goli la kwanza katika mechi ya ushindi vs Cadiz kabla ya
kutolewa baada ya Madrid kuwaambiwa walikuwa wamecheza ‘blunder’
kumchezesha Cheryshev ambaye alikuwa na kadi – ambazo alipata wakati
akiwa kwa mkopo Villareal, hata hivyo Madrid wamejitetea kwamba hawakuwa
wamepewa taarifa juu ya zuio hilo kwa mchezaji wao – lakini Fransico
Rubio, mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya soka Hispania amegoma
kusikiliza utetezi huo wa Madrid.
Madrid pia wanaamini kwamba mchezaji husika ilibidi ataarifiwe juu ya
kufungiwa kwake kabla ya mchezo na sasa inaonekana wazi klabu hiyo
itakata rufaa juu ya uamuzi huo baada ya Raisi wa klabu hiyo Florentino
Pérez alisema jana kwamba wanaangalia uwezekano wowote wa kisheria ili
kesi hiyo washinde.
Uamuzi huu wa kamati ya mashindano umezidi kumeongezea presha kocha
Rafael Benitez ambaye wadau wengi wamekuwa wakimlaumu kwa uamuzi wa
kunchezesha Cheryshev bila kuangalia kama hakuwa na shida yoyote.
No comments:
Post a Comment