31 October, 2015

Rihanna apata dili la bilioni 54 kutoka kampuni ya simu ya Samsung

rihanna
Rnb staa Rihanna ambaye kwa sasa yupo kwenye matayarisho ya mwisho ya kutoa album yake mpya ya ANTI amepata dili kubwa la kampuni ya Simu ya Samsung.
Rihanna ametia wino dili lenye thamani ya dola milioni 25 ambayo ni kama bilioni 54 za Tanzania ili Samsung wapate nafasi ya kudhamini Album yake na ziara atakazofanya Rihanna katika kutangaza album hio.
Jay Z na meneja wa Rihanna ‘Jay Brown’ walikuwa na mchango mkubwa kwenye kufanikisha dili hilo.
Rihanna atatumika kupromote biashara za Samsung kama Galaxy na mashabiki watatuma video za show za Rihanna kwenye App ya Samsung ya Milk Music App.
Hii sio mara ya kwanza Samsung kufanya kazi na Roc Nation, awali walidhamini album ya Jay Z ‘Magna Carta.. Holy Grail’ na waliisambaza kupitia simu za Galaxy.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...