05 August, 2015

WASHAMBULIAJI WATANO WANAOTEGEMEWA KUFANYA MAKUBWA EPL 2015/16

dara ya ushambuliaji inawezekana ndiyo idara muhimu sana na inayoangaliwa na watu wengi sana uwanjani, sina maaana kuwa soka linachezwa sehemu ya mbele pekee la hasha…., soka linachezwa klia kona ya uwanja ila wazungu hawakuwa wapuuzi waliposema “Striker life is in the goal scores”, wakiwa na maana kuwa maisha ya mshambuliaji yapo katika ufungaji, ukiwa mshambuliaji bila shaka assist ni kitu cha ziada ila kazi yako wewe ni kufunga tuu. Kutokana na hayo sio vibaya leo tukitazama baadhi ya wachezaji ambao baadhi ya mashabiki na wachambuzi mbalimbali wa soka wanategemea makubwa kutoka kwao kwenye idara ya kutikisa nyavu msimu ambao pazia lake tayari limefunguliwa juzi kwenye mchezo wa ngao hisani kwa “mbwatukaji” kupata kipigo kitakatifu kutoka kwa “Petit” Wenger. Naomba tuungane pamoja hapa chini kutazama washambuliaji watano ambao washabiki wanategemea kupata magoli Zaidi ya 19 kutoka kwao msimu ujao…….
5> Aleksandar Mitrovic
Mitrovic
Mashabiki wengi wa Epl wanatarajia mshambuliaji mpya wa Newcastle aliyesajiliwa kwa Euro 12M kutoka Anderlech ya Ubelgiji, Aleksandar Mitrovic kufanya makubwa kwenye ligi yenye ushindani barani Ulaya, matarajio haya yanakuja kutokana na kiwango alichokionyesha Mserbia huyu kwenye mechi ya Champion League msimu uliopita pale timu yake iliposawazisha magoli matatu dhidi ya Arsenal. Huyu jamaa alianza kupata uzoefu mapema kabisa tangu akiwa na umri wa miaka 20. Msimu uliopita alifunga magoli 20 katika ligi na kuwa mfungaji bora kwenye ligi ya ubelgiji. Pia katika mechi 69 alizocheza amefunga jumla ya magoli 36, ikiwa ni wastani wa karibu goli 1 katika mechi 2. Kutokana na kiwango chake, timu za Roma na Porto zilionyekana kuvutiwa naye sana ila mwisho wa siku alitua Saint James Park.
4> Harry Kane
Tottenham Hotspur's Harry Kane celebrates scoring his side's first goal of the game during the Barclays Premier League match at White Hart Lane, London.
clays Premier League match at White Hart Lane, London.
Hatimaye baada ya Roberto Soldado kuonekana kufanya vibaya katika idara ya ufungaji, Mauricio Pochettino aliamua kumpa nafasi kinda wa kiingereza Harry Kane na kufunga magoli 21 msimu uliopita na miongoni mwa magoli hayo ni yale aliyowafunga wapinzani wao wa London, Chelsea na Arsenal. Kutokana na kiwango chake msimu uliopita ni wazi tayari Kane ameshawafahamu mabeki wa Epl na jinsi ya kukabiliana nao. Idadi ya magoli inatarajiwa kuongezeka msimu ujao kwani utakuwa mnafiki kama ukiambiwa utaje wamaliziaji wazuri kwa sasa pale Epl alafu ukamuacha kinda huyu wa miaka 22. Tottenham itakuwa na ratiba nzuri kwani katika mechi 6 itakazo anza watakutana na timu moja pekee katika zile 8 zilizomaliza juu msimu uliopita. Hapa Kane ndo mahali ambapo anatarajiwa kuwaonea Mabeki wa timu hizi na kuanza kuweka akiba ya magoli mapema kabisa.
3> Wayne Rooney
rooney
Kuondoka kwa Robin Van Persie na Radamel Falcao, kunamfanya Wayne Rooney mpaka sasa kuwa tegemeo la Manchester United kule mbele hasa kutokana na United kutopata mshambuliaji wa kueleweka mpaka sasa japokuwa dirisha la usajii bado halijafungwa. Usajili wa viungo makini Schneiderlin na Schweinsteiger bila shaka utaimarisha idara ya kiungo na kumpa nafasi Rooney kucheza sana pale mbele na kuwa na uwanja mpana sana wa kufanya makubwa katika ufungaji. Tayari LVG ameshampa uhakika wa kuanza kila mechi kutokana na yeye kuwa nahodha wa timu. Kumbuka aliwahikufunga magoli 27 msimu wa 2011/12 na pia alitupia magoli 26 kwenye msimu wa 2009/10, misimu yote hiyo alipewa majukumu ya kucheza kama namba 9. Endapo LVG atafanya hivi ni wazi kuwa mfumo wowote atakao utumia na Rooney kucheza mbele bado atafanikiwa kupata magoli anayo yahitaji ili kuwa mshambuliaji wa pili kuwa na magoli mengi pale Epl.
2> Diego Costa
costa
Mshambuliaji hatari wa Ki Brazil anayecheza timu ya taifa ya Spain, Diego Costa”The governor”, anatarajiwa kumaliza msimu na magoli Zaidi ya 25 kama hatopata majeraha ya mara kwa mara kama msimu uliopita. Msimu uliopita alifunga magoli 20 katika mechi 26 kwenye msimu wake wa kwanza wa Epl, endapo kama sio Majeraha ni wazi hakuna mtu ambaye angemkamata Diego katika ufungaji wa EPL, kumbuka hakuwa na goli hata moja la penati katika magoli yake yote. Kutokana na support atakayo ipata kutoka kwa viungo wakabaji na washambuliaji ambao siku zote wapo nyuma yake, Oscar, Hazard na Willian ni wazi Diego ataendelea kupata huduma nzuri na kutupia nyavu mara kibao, pia assist za Cesc zitazidi kumuweka juu mchezaji huyu ambaye mpaka sasa hajafahamu lugha ya kiingreza licha ya kukaa takribani mwaka mzima pale London. Kumbuka Chelsea itakutana na Man City pamoja na Arsenal katika mechi 6 za mwanzo. Endapo diego atakuwa fiti bila majeraha naamini ataanza vizuri katika mechi hizi
1> Sergio Aguero
aguero
Hatutaweza kushangaa endapo Jamaa lenye nguvu na kasi kutoka Argentina, Sergio Aguero kuwa mfungaji bora wa ligi kwa mara nyingine tena. Amekuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga kwenye michuano ya Copa America baada ya kufunga magoli 3 katika mechi 5, kumbuka msimu uliopita alimaliza na magoli 26 katika mechi 33 huku akitoa assist 10. Kutokana na kiwango chake ni wazi Aguero atakuwa na msimu mwingine mzuri hasa kutokana na kuwa mzoefu kwenye Epl kwa muda sasa, kingine pia huyu jamaa ndo mpiga penati za ndani ya uwanja hivo bado ana faida ya kuzidi kuongeza magoli hasa baada ya usajili wa Raheem ambaye anapenda ku drible hadi kwenye box za wapinzani.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...