Kocha mkuu wa klabu hiyo Jamhuri
Kihwelo ‘Julio’ amesema pamoja na kukamilisha usajili wa wachezaji
waliokuwa wanawahitaji, lakini bado nafasi ipo kwa ajili ya Juma Kaseja
na Jerry Tegete kwani wakipewa nafasi wanaweza wakaonesha uwezo mkubwa.
“Mimi nimeshamaliza usajili,
nimeshasajili wachezaji 26 wanatosha, wachezaji pekee ambao kama mipango
yangu itaenda sawasawa basi kuna mpango wa kuwaongeza Juma Kaseja na
Jerry Tegete. Kwasababu ni wachezaji ambao nimezungumza nao na
wameniambia wanataka kucheza na hawakuweka mbele kipato, mimi
wamenivutia kwasababu tunapokuwa na wachezaji kwenye timu tunataka
tuwatumie kucheza ili tupate mafanikio kwenye ligi”.
“Lakini
kunawachezaji ambao hawaperfom inabidi tuwatoe kwenye dirisha dogo la
usajili, lakini ukiwa na wachezaji wazuri wenye kuonesha commitment
ambao wanataka kucheza kuisaidia timu yao sioni kwanini nisiwachukue
kwasababu namba bado inatosha”.
Kwa usajili wa wachezaji wa
kigeni unaofanywa na baadhi ya vilabu vya ligi kuu hapa nhini Julio
amesema yeye hatishwi na usajili huo kwani yeye ni Kocha mkubwa na
anatambua uwezo wa wachezaji wengi na hata pale anapowaita wachezaji
haoni kama ni wazee na anatambua kuwa ni wachezaji wenye uwezo mkubwa”.
“Mimi kwanza sitishiki na usajili
wa Azam, Simba na Yanga, wao wamevutika na wachezaji wao wa nje
kwasababu zao binafsi kwanza wanafedha,Yanga wanatarajia wakiwa na
wachezaji wa kigeni watafanikiwa kwasababu wanacheza mashindano ya
Afrika wanataka kuingia kwenye ‘Super eight’ ili wafanikiwe. Mimi
sidhani kama hilo litafanikiwa”.
Lakini Azam hivyohivyo nao
japokuwa juzi wamechukua ubingwa wamefanya vizuri nimeona timu yao sio
mbaya sana, Simba wamepoteza ubingwa kwa takribani miaka mitatu kwahiyo
wanategemea wakiwa na wachezaji wa nje basi wanaweza wakafanya kile kitu
wanachokitarajia na watapata ubingwa lakini sioni kama itafanikiwa
vilevile”.
Msikilize Julio hapa chini akieleza nia yake ya kuwasajili Kaseja na Tegete
No comments:
Post a Comment