19 August, 2015

Wanajeshi 8 wa Uturuki wauawa


Wanajeshi wanane wa Uturuki wameuawa kwenye shambulizi la bomu la kutegwa kando ya barabara kusini mashariki mwa nchi.
Hakuna kundi lililodai kuhusika kwenye shambulizi hilo lilitokea katika mkoa wa Siirt lakini maafisa wa usalama wamewalaumu waasi wa PKK au kundi la Kurdistan Workers Party.
Shambulizi hilo linafanyika wakati kuna ghasia kati ya PKK na wanajeshi wa Uturuki. Watu kadha wameuawa tangu usitishwaji wa mapigano wa miaka miwili uvunjike mwezi Julai.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...