Uongozi wa klabu ya Simba leo
umetoa zawadi kwa washindi wa bahati na sibu iliyochezeshwa siku ya
Simba Day Aosti 8 mwaka huu wakati wa kilele cha sherehe za siku ya
Simba Day zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Zawadi zilizo kabidhiwa kwa
washindi ni jezi pamoja simu, kila mshindi amepata jezi ya juu pea moja
pamoja na simu moja aina ya Motec. Washindi wa zawadi hizo ni Jeremia
Venist, Ahazi Mwembe pamoja na Marko Mgimba.
Mbali na zawadi hizo, klabu hiyo
pia imekabidhi mipira nane kwa shule mbili za msingi za mkoa wa Dar es
Salaam ambapo Shule ya Msingi Mikocheni A imepata mipira minne huku
Shule ya Mingi Chang’ombe Mazoezi nayo ikikabidhiwa mipira minne.
Rais wa klabu ya Simba Evans
Aveva amesema, klabu hiyo inataka kusaidia soka la vijana nchini na
kwasasa wameanza na mkoa wa Dar es Salaam lakini baadae watasonga mbele
hadi kwenye mikoa mingine ili kuwafikia watu wengi zaidi hasa watoto
ambapo ndio leno hasa la klabu hiyo kusaidia soka la vijana.
No comments:
Post a Comment