Wakiwa huko, Yanga tayari wamecheza mechi mbili za kirafiki ambapo ya kwanza walishinda 4-1 dhidi ya Kimondo FC.
Magoli ya Wanajangwani katika
mchezo huo uliopigwa uwanja wa CCM Vwawa Mbozi yalifungwa na Geofrey
Mwashiuya (mawili), Simon Msuva na Amissi Tambwe.
Yanga jana imecheza mechi
nyingine dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine ambapo ilishinda
2-0, magoli yakifungwa na Malimi Busungu na Amissi Tambwe.
Jumapili ya wiki hii, Yanga watakabiliana na Mbeya City uwanja huo wa Sokoine.
No comments:
Post a Comment