Siku za karibuni Darren Urquhart na Tom Smith wameanzisha project moja ambayo wameipa jina la “Bad Boys FC”.
Wawili hao wamekumbushia baadhi ya matukio makali yaliyowahi kutokea katika ulimwengu wa soka ambapo wamewahusisha watoto.
Project hiyo imetumia baadhi ya picha zisizosahaulika katika mchezo wa soka.
Urquhart na Smith walieleza kwamba, wameamua kufanya hivyo ili kuona kama wanamichezo wa sasa wanaweza kuigwa na vijana katika soka la England, wakati huu kuna mishahara mikubwa na maisha mazuri kwa mastaa wa kandanda.
Hapa chini ni picha kutoka project ya Bad Boy FC
1. Why Always Me – Mario Balotelli.
Hii haitasahaulika na hapa wamewahusisha watoto ambao
wameigiza tukio hilo, huku mmoja akiigiza kama nyota wa Manchester
United, Anderson na Man City, David Silva.
2. Tiny Hand of God – Diego Maradona
Hili ni goli la Mkono wa Mungu alilowahi kufunga Diego Maradona, hakika watoto kwa asilimia mia wameigiza kuanzia namna alivyoweka miguu.
3. Baby Teeth – Luis Suarez
Tukio hili la Luis Suarez kumng’ata Branislav Ivanovic nalo wamejitahidi kuliigiza hapa chini;
4. Kicking & Screaming – David Beckham
Tukio hili ambalo lilifanywa na Beckham nalo limeigizwa na watoto
5. My Mum’s a What?! – Zinedine Zidane
Hili ni tukio alilofanya Zidane dhidi Marco Materazzi wa Italia.
6. Karate Kid – Eric Cantona
Cantona aliwahi kumshambulia shabiki kwa Kareti, huku
mwanamke mmoja kulia akionekana kushangaa. Hapa wamejitahidi kukumbushia
tukio hilo.
7. Learn to Play Nice- Martin Keown
Hili ni tukio la Keown na Ruud van Nistelrooy
No comments:
Post a Comment