11 August, 2015

UEFA SUPER CUP: BARCELONA KUWAKOSA NYOTA HAWA DHIDI YA SEVILLA USIKU WA LEO..

Barcelona vs Sevilla Uefa Super Cup 2015 Predictions
Miamba ya kandanda nchini HISPANIA, FC BARCELONA na SEVILLA inakabiliana usiku huu katika fainali ya UEFA SUPER CUP inayopigwa BORIS PAICHADZE DINAMO ARENA, MJINI TBILISI, GEORGIA
Mchezo huu unaowakutanisha Mabingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI na waliobeba UEFA EUROPA LIGI, ndio unaoashiria kuanza rasmi kwa Msimu mpya wa Soka Barani Ulaya.
Mechi hii ya kusisimua inaanza kupigwa kuanzia Saa 3 Dakika 45 Usiku huu kwa saa za Afrika mashariki.
FC Barcelona wanatinga Uwanjani bila ya nyota wake wa Brazil Neymar,  huku wakisaka kuifikia rekodi ya AC Milan ya kutwaa mara tano UEFA Super Cup.
Mbali ya kumkosa Neymar, ambaye nafasi yake inachukuliwa na Pedro anayedaiwa kuhamia Manchester United baada ya Mechi hii, Barca, chini ya Kocha Luis Enrique, pia inawakosa majeruhi Jordi Alba na Douglas.
Wachezaji wapya,  Arda Turan na Aleix Vidal hawaruhusiwi kucheza hadi Januari kwa vile hivi sasa Barca ipo kwenye Kifungo cha FIFA cha kutosajili.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Sevilla kugombea UEFA Super Cup baada ya kutetea vyema Taji lao la EUROPA LIGI lakini Mwaka Jana kwenye Fainali hii walichapwa magoli mawili kwa bila dhidi ya Real Madrid.
Sevilla, chini ya Kocha Unai Emery, hawajaifunga Barcelona katika Mechi 19 ingawa safari hii wana nguvu mpya ya Wachezaji wapya , YEVHEN KONOPLYANKA na CIRO IMMOBILE

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...