09 August, 2015

Kilichowakuta Arsenal dhidi ya West Ham

Ligi kuu ya Uingereza Baclays Premier imeendelea jumapili ya leo kwa mchezo uliowakutanisha mahasimu wa mji wa London – Arsenal dhidi ya West Ham United.
 
Mchezo huo uliomalizika hivi punde umemalizika kwa West Ham United kuwashangaza watu wengi kwa kuifunga Arsenal kwa magoli 2-0.
 
Koyaute alianza kuifungia goli West Ham katika dakika ya 43 ya kipindi cha kwanza, kabla ya Zarate kufunga goli la pili na kuhitimisha ushindi muhimu dhidi ya vijana wa Arsenal Wenger.
 
Wakati huo Newcastle United imetoka sare ya 2-2 dhidi ya Southampton.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...