06 August, 2015
Diamond na Zari wajaliwa mtoto wa kike
Msanii wa Bongo mwenye umaarufu wa kimataifa, Diamond Platnumz, maarufu, Naseeb Abdul, amepata majukumu mapya baada ya kujaliwa mtoto. Mkewe msanii huyo, Zarina Hassan, Zari the boss lady, alijifungua msichana mapema leo na kuipa furaha familia hiyo.
Baada ya kuokota tuzo tofauti kwenye mziki, Diamond hatimaye amepata tuzo kutoka kwa Mungu kwa kufanya juhudi nyingi za kutaka kuwa mzazi.
Diamond alipachika picha ya mtoto wake akibebwa na mamake, Sanura Kassim kwenye ukurasa wake wa Instagram na kupokea pongezi kutoka mashabiki.
Aidha, msanii huyo amemuanzishia mtoto wake ukurasa wa Instagram kwa jina Tiffah Dangote na kuvutia zaidi ya wafuasi elfu kumi na sita.
Diamond mwenye umri wa miaka 25, aliwashangaza wengi kwa kuanza kumfanyia bintiye ununuzi wa vifaa vya watoto kabla ya kuzaliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment