04 August, 2015

MIAKA 20 YA WENGER: FAHAMU VITU KIBAO USIVYOVIJUA KUTOKA KWA “PROFESSOR” WENGER

wengerKuna Msanii mmoja kutoka pale nchi yenye maandishi matatu sikumbuki
jina lake ila nahisi kama linafanana na Shilingi 50…! Nasikia jamaa
anaelekea kufilisika..! Duuuh..! Kweli hali korofi ila kipaji chake
kitambeba na hatimaye zile fulana zake “Masharaboro” wataanza kuvaa
tena na nyimbo kama “Candy shop” zitarejea tena…!! Anyway tuachane
na hayo ila lengo langu kuanza na stori ya huyo jamaa ni kujaribu
“ku-link” uwezo wa Kocha wa sasa wa Arsenal Mzee Arsene Wenger..! Je,
ipo siku uwezo wake utarudi nyuma na kufilisika kisoka? Mimi na wewe
hatuwezi fahamu ila Wazungu wanasema “Lets wait & see”…..!
Msimu ujao Kocha mkongwe kwa sasa pale Epl kutoka taifa la Ufaransa,
Mzee mwenye umbile dogo asiependa shari na mtu, kutokana na umbile
lake alipewa jina la utani la “Petit” likiwa na maana ya Dogo. Kocha
huyu ndo Meneja aliye iongoza Arsenal kwenye mechi nyingi zaidi mpaka
sasa, pia aliwahi kuwapa ubingwa “Ze gunner” Bila kupoteza mechi..!
Ili kupata mengi zaidi ungana na mimi hapa chini kufahamu mengi kutoka
kwa Kocha huyu ambaye pengine hukuwahi kufahamu ama kufikiri kuwa yana
muhusu Arsene Wenger….
ARSENE WENGER KACHEZA SANA “NDONDO”.
Kabla ya kufikisha miaka 29 ambapo ndo alipoanza kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Rc
Strasbourg na kuchukua ubingwa wa Ligue 1 mwaka 1978, huwezi amini
Wenger alitumia muda wake wote hapo nyuma kucheza soka mtaani kabla ya
kwenda Mutzig ambapo alikuwa anacheza kama beki, “Style” ya uchezaji
wake inafananishwa na beki wa Kifaransa anaecheza Chelsea kwa sasa
Kourt Zouma, alikuwa anapenda kuosha na kubutua mipira sana. Alistaafu
soka akiwa na miaka 32 mara baada ya kuchukua ubingwa wa Ligue 1 mwaka
1978. Baba yake pia alikuwa kocha wa klabu ya mtaani kwao.
WENGER NI MSOMI MWENYE DEGREE YA UCHUMI.
Hatimaye alipata taaluma hii katika Chuo Kikuu cha Strasbourg baada ya kujiunga 1971. Pia mbali na
Uchumi amesomea pia mambo ya siasa na alianza taaluma yake ya ukocha
pindi alipostaafu kwa kuwafundisha wachezaji wa kikosi cha pili na
timu ya vijana ya Rc Strasbourg. Taaluma hii ya uchumi ndiyo
inayomuhusisha Wenger na ubahili wa kusajili wachezaji kwa pesa ndogo.
Pia alijifunza lugha ya Kingereza kwenye kozi ya wiki 3 pale Cambridge
na kufahamu lugha hiyo kwa haraka zaidi. Kweli huyu mzee ni Genieus.
BABA YAKE MICHEL PLATINI AMPA SHAVU.
Wakati Wenger akiwa Kocha msaidizi pale Ligue 2 kwenye klabu ya As Cannes 1983, msimu uliofuata
Aldo Platini, Baba yake na rais wa Uefa Michel Platini alishauri
Wenger akafundishe ligi kuu kwenye klabu ya Nancy. Msimu wake wa
kwanza Wenger alimaliza nafasi ya 12..! Hapa ndo unagundua huyu Mzee
ni “Genius” tangu kitambo. Badae timu hii ilimtelekeza kwa dharau Mzee
Wenger ikiwa ni kipindi cha msimu mmoja pekee tangu ajiunge nayo.
KAFANYA KAZI YA UKOCHA BARANI ASIA.
Mnamo 1995, mwaka mmoja baada ya beki anaecheza kama yeye kuzaliwa {Kourt Zouma}, Wenger aliajiriwa
kuifunza timu ya Nagoya Grampus Eight ya Japan. Alifanya kazi Japan
kwa miezi 18 kwa mafanikio makubwa na alipata tuzo ya Kocha bora wa
mwaka kwenye msimu wake wa kwanza. Pia kabla ya kuondoka Japan
aliiacha timu hii ikimaliza nafasi ya pili kwenye ligi.
WENGER ANAZUNGUMZA LUGHA SABA TOFAUTI.
Watu wengi wanajua zile lugha 6 pekee za hapo awali, ila ukweli ni kwamba lugha ya Kichina imeongezeka
kwenye zile lugha zingine 6 ambazo ni Kifaransa, Kijerumani,
Kingereza, Kihispania, Kitaliano na Kijapan. Hapa ndo jina la utani la
“Profesa” lilipoanzia. Huyu Mzee ni Genius sana..! Em niambie nani
mwingine anaweza kufanya kama hivi.!!! Teh teh teh teh tegemea siku
moja kumuona anachambua mpira kwa kilugha ya Kichina kwenye World Cup
ya 2018..!
DAVID DEIN KAMPIGIA CHAPUO.
Huyu jamaa alikuwa Makamu Mwenyekiti wa
Arsenal ambaye alikutana na Wenger 1988 kwenye mechi dhidi ya Qpr na
wakajenga urafiki. Mzee Wenger akiwa mshauri wa ufundi wa Fa, Dein
alimpigia chapuo Wenger kuifundisha Arsenal na hatimaye mwaka 1996
September 30 aliajiriwa rasm kama Meneja wa “ze gunners”
KAMUOA MCHEZAJI WA MPIRA WA KIKABU.
Mwanamama Annie Brosterhous mchezaji wa mpira wa kikapu na mara baada ya kuwa wanandoa, Mzee
Wenger alimuahidi Mkewe kuwa atafundisha soka kwa miaka 5 pekee na
baada ya hapo atastaafu..! Mpaka sasa Profesa Wenger hana hata dalili
ya kustaafu…. Teh teh teh teh watoto wa mjini wanasema Wenger
alikuwa anatafuta “Gear” ya kukubaliwa na Mrembo huyu. Mpaka sasa wana
binti anaitwa Lea, alizaliwa 1997.
WENGER NDIYE ALIYEMFUNGULIA MLANGO GEORGE WEAH.
Mnamo mwaka 1988 Wenger alipigwa “madongo” sana kwa kumsajili Mwafrika ambaye
hafahamiki kwenye klabu ya Monaco, jina lake ni George Weah kutoka
taifa la Liberia, miaka 7 baadae Wenger akiwa Japan kikazi, Weah akawa
mchezaji bora wa dunia. Aibu ikawajaa waliokuwa wanampiga wenger
“madongo”. Kumbuka hata usajili wa Henry kutoka Juve ulipigiwa kelele
sana kuwa Mzee Wenger kachemsha, baadae Henry alitupia magoli zaidi ya
256..! Mwacheni Babu Wenger aitwe Genius…!
MUUMINI WA VYAKULA VYA KIJAPANI.
Mzee Wenger anapenda sana wembamba na mara nyingi amekaririwa akisema anapenda vyakula na maumbile ya watu
wa taifa la Japan kwa sababu vyakula vyao ni Mboga za kuchemsha,
Samaki, Mchele na hawatumii Sukari wala mafuta…! Kutokana na haya
Profesa Wenger anapenda sana vyakula vya Kijapan. Pia hapendelei
wachezaji wenye miili mikubwa kama akina Charlie Adam.
ALIWATEMBELEA WAZAZI WA GAEL CLICHY NA PHILLIPE SENDEROS KUWAOMBA
WAWARUHUSU WATOTO WAO KWENDA LONDON.
Mbali na Mzee Wenger kwenda nyumbani kwa akina fundi Cesc Fabregas, pia aliwahi kwenda Ufaransa
kwa akina Clichy na Uswis kwa akina Senderos kukutana na wazazi wa
wachezaji hawa..! Niambie Kocha mwingine aliyewahi kufanya hivi..!
Babu Wenger yupo tofauti kidogo na wengine.
ALITUMIA £6 MILIONI KUWEKA REKODI.
Mwaka 2006 Profesa Wenger aliweka rekodi ya kucheza mechi 10 za Uefa bila kuruhusu goli huku safu yote
ya ulinzi ikitengenezwa kwa Euro millioni 6.
KATWAA TUZO YA KOCHA BORA WA KIPINDI CHA MIAKA 10.
Kuna taasisi kubwa inayoheshimika duniani inaitwa International Federation of Football
History and Statistics, taasisi hii ilimpa tuzo ya kocha bora wa
kipindi cha miaka 10 mnamo mwaka 2011. Kumbuka taasisi hii iliwahi
kuichagua timu ya Sevila kama klabu bora duniani mwaka 2006 na 2007.
KAPANGA KIKOSI BILA KUWA NA MCHEZAJI WA KI-INGEREZA.
Akiwa anafundisha timu ya Waingereza, mnamo mwaka 2005 siku ya “Valentine day” akiwa
anacheza dhidi ya Crystal Palace alipanga kikosi cha wachezaji 16
ambao wote walikuwa ni wageni.
KIPIGO KITAKATIFU KWENYE MECHI YAKE YA 1000.
Akiwa anaiongoza klabu yake kwenye mechi ya 1000 dhidi ya Chelsea mnamo tar 22 March 2014,
Wenger alipata kipigo kitakatifu tena cha mbwa mwizi kutoka kwa Kocha
“mbwatukaji” Jose Mourinho. Ni miongoni mwa mechi ambazo hawezi
kuzisahau ikiwemo na ile ya magoli 8-2 kutoka kwa Babu Ferguson

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...