Terry (34) alikuwa ni nguzo imara
ya Chelsea wakati wa msimu uliomalizika akikiongoza kikosi hicho kutwaa
ubingwa wa ligi ya England (EPL) kwa mara ya kwanza tangu walipofanya
hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2010.
Ubora aliouonesha Terry ulimfanya
atajwe kuwa kwenye kikosi cha PFA kwa msimu uliopita ikiwa ni mara ya
kwanza tangu alipotajwa kwenye kikosi hicho kwa mara ya mwisho msimu wa
2005-06.
“Nilipokuja, nilikuja na swali:
Nitamkuta John wa aina gani? Atafanya nini? Ataimarika? Atamkaribia John
yule ninaemfahamu mimi?” Mourinho aliuambia mtandao wa ESPN.
Kabla ya ujio wa Mourinho 2013,
hatma ya Terry ilikuwa mashakani ndani ya Stamford Bridge na alikuwa na
wakati mgumu wakati wa utawala wa Rafa Benitez.
Mchezaji huyo wa zamani wa kikosi
cha England alianza kwenye mechi 24 kati ya 69 ambazo Chelsea ilicheza
kwenye mashindano yote kwa msimu wa 2012-13. Mourinho akaongeza kuwa
hakujua kuwa, ubora wa beki huyo ulikuwa uko mikononi mwake.
“Hususan kabla sijaja wakati wa
kipindi cha Rafael Benitez nilidhani huyu mtu amekwisha kwasababu
alikuwa hachezi mechi kubwa nikafikiri atakuwa kwenye matatizo”.
Chelsea wanaanza mapambano ya
msimu mpya mwishoni mwa juma hili kwenye dimba la Wembley, wakati
watakapopambana na Arsenal kuwania taji la kwanza la ngao ya jamii.
Chelsea imepata nafasi hiyo ya
kucheza mchezo wa ngao ya jamii baada ya kushinda taji la ligi kuu ya
England wakai Arsenal wao walishinda kombe la FA.
No comments:
Post a Comment