01 August, 2015

“Kuacha Aina Ya Muziki Uliokutambulisha Unakuwa Haupo Loyal Kwa Mashabiki Wako” – Mansuli

man 
Msanii wa hip hop, “Kina kirefu” rapper Mansuli amefunguka na kusema kwamba msanii kuacha aina ya muziki uliokutambulisha wakati unaanza kufanya unakuwa haupo loyal kwa mashabiki wako unakuwa hauwatendei haki watu wako, ingawa kila mtu anakuwa na uhuru wa kufanya kitu ambacho anakipenda.
Mansu,I ni moja ya wasanii wanaofanya hip hop halisi, ameendelea kufanya hivyo toka alipoingia kwenye game, toka ngoma ya “Kina kirefu” ilipomtambulisha katika gemu, ameendelea kupewa heshima ndani ya gemu la hip hop.
Kwa sasa Mansulii amerudi rasmi baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na masomo, leo Jumamosi ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la “Usiku Mmoja” feat Maulo, ngoma ambayo imefanywa na producer Pala kutoka Tatoo Records Masaki Dar es salaam.
Anafanya mipango ya kufanya video ya ngoma na mkali Director Hanscana, akiamini kwamba directors 1a Tanzania pia wao wanaweza, akiongelea kuhusu video kupigwa Tv za kimataifa kwa nyimbo za Kibongo amesema ni kitu kizuri.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...