05 August, 2015

ANGEL DIMARIA ATAJUTIA KWA YALIYOTOKEA

DI MARIAWakati Manchester United ikimsajili mchezaji Angel Di maria kutoka Real Madrid msimu uliopita, kila mmoja alidhania kuwa wamepata professional na mchezaji wa kiwango cha dunia.
Real Madrid walijitahidi kadiri ya uwezo wao kumzuia asiondoke mchezaji huyo aliyekuwa uti wa mgongo katika kufanikisha ‘La Dacima’ kombe la kumi la UEFA champions league, lakini tayari Dimaria alikua kaisha itengeneza akili yake kuondoka huku akiviamsha usingizini vilabu vya Manchester United na PSG kuwania saini yake.
PSG ndio waliokuwa kipaumbele kumsaini lakini Real Madrid walikataa kumkopesha baada ya PSG kubanwa na sheria ya matumizi ya pesa ya UEFA, financial fair play. Hatua hiyo ikampa faida Ed Woodward kumleta Old Trafford kwa ada ya pauni 60m. Hapa mambo hayakwenda sawa kwa Dimaria na bila shaka anatamani asahau haraka.
Kwanza, Dimaria alitua Old Trafford na kukabidhiwa jezi namba 7 ambayo katika historia ya klabu ya Manchester United, ina matarajio makubwa sana na Dimaria akashindwa kuitendea haki.
Pili, Dimaria alikuja Old Trafford kwa ada kubwa kabisa ya uhamisho na kuweka rekodi ya klabu na ligi kuu nchini England. Ada ya pauni 59.7m na sasa anaondoka kwa pauni 44.4m ni dhihaka kubwa kwa Dimaria mwenyewe na hasara kwa klabu.

Tatu, ahadi na maneno yake mazuri ya kutua Old Trafford vyote vimeyeyuka. Dimaria aliwahi kusema Manchester United ingekua timu yake ya mwisho kuichezea barani ulaya kabla ya kurudi kwao Argentina. Leo hii amejikuta akichukiwa sana na mashabiki wa Manchester United na pia ni doa katika CV yake.
Mwisho, mashabiki na klabu zinastahili kulipwa fadhira zao kutoka kwa wachezaji. Wachezaji pia wanatakiwa kuishi kiume na kusema wazi wazi hisia zao ili wasijikute wanawakera mashabiki zao na kuzipa hasara klabu. Dimaria anajikuta mnafiki na mtu asiye mueledi kutokana na yote yaliyomtokea katika career yake hadi hivi sasa.
Hatimaye yote niliyoyaandika hapo juu yana madhara makubwa kabisa katika maisha ya Dimaria aidha kiakili ama kimwili. Zaidi ya mashabiki 650m wa Manchester United duniani kote, sasa wanamchukia Dimaria na hilo litamtesa mchezaji huyo. Atajutia sio tu kuondoka United, bali Real Madrid.
Real Madrid ndio wanaoendelea kummiss zaidi kwani alikuwa mmoja wa waliokuwa uti wa mgongo wa timu na hata pengo lake linaonekana tofauti na Manchester United ambako hakua na msaada wowote.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...