Sio zaidi ya siku tatu zimepita toka kocha wa Manchester United Louis van Gaal athibitishe kutokujua wapi alipo kiungo wa Kiargentina Angel Di Maria baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari juu ya kutoonekana kwake kikosini kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Uingereza.
Kutoonekana kwake kikosini inadaiwa ni ishara ya Di Maria kushinikiza uhamisho wake wa kwenda katika klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa baada ya kuhusishwa kujiunga nayo kwa muda mrefu.
August 2 taarifa mpya zimetoka zinazobainisha mpango wa Di Maria kuhamia katika klabu ya PSG
kuwa klabu hizo mbili zimefikia makubaliano ya kuuziana kiungo huyo kwa
pound milioni 44.5 na atafanya vipimo vya afya jumapili ya August 2
kabla ya kusaini mkataba na klabu hiyo.
Angel Di Maria akiwa na Manchester United amecheza mechi 32 katika mashindano yote na kufunga magoli 4 na assist 12, kocha wa klabu ya PSG Laurent Blanc amethibitisha klabu yake kuwinda saini ya Di Maria kwa zaidi ya misimu miwili na atafanyiwa vipimo vya afya Qatar.
No comments:
Post a Comment