02 August, 2015

KCCA YAITWANGA KHARTOUM NA KUSHIKA NAFASI YA TATU KAGAME

KCC VS KNCTimu ya KCCA FC imefanikiwa kuwa mshindi wa tatu wa michuano ya CECAFA Kagame Cup kwa mwaka 2015 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1dhidi ya Khartoum National Club kwenye mchezo uliochezwa mchana kumtafuta mshindi wa tatu kufuatia timu hizo kufungwa kwenye michezo yao ya nusu fainali na kuangukia kucheza mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu wa mashindano hayo.
Magoli ya KCCA yamefungwa kipindi cha kwanza na Birungi Michael na Mutyaba Muzamiru wakati goli la kufutia machozi kwa Khartoum likiwa limefungwa na Ousmaila Baba kipindi cha kwanza pia.
Birungi Michael wa KCCA na Ousmaila Baba wa Khartoum walijikuta hawamalizi kipindi cha kwanza bada ya kuoneshwa kadi nyekundu baada ya wao wenyewe kuchezeana rafu na mwamuzi wa mchezo Martin Sanya wa Tanzania kuwatoa nje kwa kai nyekundu.
KCCA ambao ndio washindi wa tatu wamenyakua kitita cha dola za kimarekani 10,000 kama zawadi ya kumaliza wakiwa nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...