10 August, 2015

Diamond na Vanessa Mdee watajwa kuwania tuzo za Canada

Diamond Platnumz na Vanessa Mdee wameendelea kupata nominations za tuzo za kimataifa. Wawili hao walioiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za MTV MAMA 2015 ambapo Diamond alishinda, wametajwa tena kuwania tuzo zingine za kimataifa zijulikanazo kama, African Entertainment Awards (AEAwards) za nchini Canada.

Vanessa ametajwa kuwania kipengele cha International Best African Female Artist ambapo atachuana na wasanii wengine wakiwemo Victoria Kimani wa Kenya na Yemi Alade na Seyi Shay wa Nigeria.

Diamond anawania kipengele cha International Best African Male Artist akichuana na AKA wa Afrika Kusini, Sarkodie wa Ghana na Olamide wa Nigeria.

Tuzo hizo za nne kufanyika zitatolewa Jumamosi ya September 5, 2015 huko Mississauga, Ontario.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...